Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 36-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Anayetokwa Majimaji Anafaa Kusoma Qur-aan Na Kuswali Swalaah Za Sunnah?

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

36-Mwanamke Anayetokwa Majimaji Anafaa Kusoma Qur-aan

Na Kuswali Swalaah Za Sunnah?

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Mwanamke akitawadha ambae hutokwa na majimaji haya kwa ajili ya Swalaah ya faradhi je ni sahihi kwake aswali anachotaka kwa ajili ya Sunnah na kusoma Qur-aan  kwa wudhu wa faradhi ile kwa ajili ya faradhi  nyingine?

JIBU:

Akitawadha kwa ajili ya Swalaah ya faradhi kwa  wakati wake wa mwanzo  basi ni juu  yake  kuswali faradhi, Sunnah au kusoma Qur-aan hadi wakati mwingine wa Swalaah nyingine.