Zurubiani (Wali Wa Ki-Saudia)

Zurubiani (Wali Wa Ki-Saudia)

 

Vipimo

Mchele - 5 mugs (kikombe kikubwa)

Nyama (au kuku) - 2 Ratili (LB)

Chumvi - Kiasi

Mafuta -  3/4 kikombe

Samli - 1/2 kikombe

Vitunguu Vikubwa  (kata virefu virefu) -  6

Nyanya (iliyosagwa) - 6 vijiko vya chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chakula

Pilipili mbichi - ½ kijiko cha chai

Hiliki nzima - 6 chembe

Mdalasini nzima - 5 vijiti

Mtindi   (yoghurt) - ½ kikombe cha chai

Karoti - 1

Mapilipili makubwa - 2  kijani na jekundu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi

  1. Kwenye sufuria mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown)
  2. Mimina nyama, abdalasini, hiliki na chumvi kwenye hiyo sufuria ya vitunguu ikaange moto wa kiasi mpaka nyama iwive.
  3. Saga ile Karoti pamoja na mtindi kwenye blender (mashine yakusagia) kisha imimine kwenye nyama
  4. Tia  nyanya iliyosagwa.
  5. Ikichemka weka moto mdogo mdogo mpaka mafuta yake yaje juu.
  6. Tia zile pilipili ulizo zikata kata rangi mbili.
  7. Yatowe mafuta yote weka pembeni.
  8. Acha sosi pee yake.

 

Wali:

  1. Osha mchele uroweke kwenye maji kwa muda wa dakika 20
  2. Chemsha maji kwenye sufuria kiasi cha magi 10
  3. Yakishachemka unatia mchele, chemsha usiive sana, unamwaga maji.
  4. Unamimina ule mchele juu ya lile rojo (sosi)
  5. Mafuta uliyoyatoa kwenye sosi yapashe moto halafu unayamimina juu ya mchele, unarudisha motoni. Unaweka motot mdogo mdogo ukisha  kuiva, tayari kupakuliwa.
  6. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.

 

 

Share