Skip to main content

05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلصِّيَامِ - Kitabu Cha Swiyaam01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swiyaam: Taarifu Ya Swawm

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

Mlango Wa Swiyaam

01-Taarifu ya Swawm

Alhidaaya.com

[Al-Lubaab (1/162), Al-Majmuw’u (6/248) na Al-Mughniy (3/84)]

الصيام و الصوم  “Swiyaam” na “HAJJ” katika lugha ya kawaida ina maana ya kujishika na kujizuia na kitu, na hutumiwa katika kujizuia kwa aina zote. Allaah Ta’aalaa Akimzungumzia Maryam (‘Alayhas Salaam) Amesema:

(( إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا))

((Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm [ya kutozungumza] kwa Ar-Rahmaan)). [Maryam (19: 26)]

Yaani, kunyamaza, kujishika na kujizuia na kunena.

Ama kisharia, ni kujizuia na vyenye kufunguza Swawm toka kuchomoza Alfajiri hadi jua kuchwa pamoja na niya ya kumfanyia ‘ibaadah Allaah Ta’aalaa.