Skip to main content

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

Alhidaaya.com

 السَّمِيعُ

السَّمِيعُ

As-Samiy’i

Mwenye Kusikia Yote Daima

Allaah (سبحانه وتعالى) Anayesikia sauti zote, katika lugha zake tofauti tofauti na zote katika wingi wake na haja mbalimbali.

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾

Watakapoamini kama vile mlivyoamini nyinyi, basi kwa yakini watakuwa wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, na Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah (2):137]

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَاللَّـهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٢٠﴾

Na Allaah Anahukumu kwa haki. Na wale wanaowaomba badala Yake hawawezi kuhukumu kwa chochote. Hakika Allaah Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ghaafir (40): 20]