Skip to main content
⌂
Alhidaaya.com homepage
slogan image
  • Log in

left sidebar menu

  • Qur-aan
  • Hadiyth
  • Sunnah
  • Tawhiyd
  • Aqiydah
  • Manhaj
  • Shirki & Kufru
  • Bid-'ah (Uzushi)
  • Salaf Wa Ummah
  • Firaq-Makundi
  • Fiqh-Ibaadah
  • Duaa-Adhkaar
  • Fataawa Za Ulamaa
  • Kauli Za Salaf
  • Akhlaaq-Aadaab
  • Raqaaiq
  • Familia-Jamii
  • Maswali-Majibu
  • Chemsha Bongo
  • Vitabu
  • Mapishi

29-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْقَدِيرُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

Alhidaaya.com

الْقَدِيرُ

الْقَدِيرُ

Al-Qadiyr

Muweza Wa Yote Daima

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Mwenye nguvu timilifu na kamilifu na uwezo. Kwa nguvu Zake Amefanya kila kitu kiwepo. Kwa nguvu hiyo Yeye hupanga kila kitu. Kwa nguvu hiyo, Ameumba na kukamilisha uumbaji. Kwa nguvu hiyo, Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Huhuisha na kufisha. Kwa nguvu hiyo Atafufua waja kwa ajili ya jazaa yao;  kuwapa malipo waliofanya mema na kuwaingiza Motoni kwa waliotenda uovu. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye, Anapotaka jambo liwe huliambia tu:

كُن فَيَكُونُ

Kun! basi (jambo) huwa!

Kwa nguvu Zake Allaah (سبحانه وتعالى) na uwezo, hugeuza nyoyo na kuzielekeza kwa yeyote Amtakaye.

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾

Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni kwenye mambo ya khayr. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Baqarah (2): 148]

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾

Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo ni kutoka kwenu wenyewe. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Aali ‘Imraan (3): 165]


Book traversal links for Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi (من) تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان

  • ‹ 28-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُهَيْمِنُ
  • Up
  • 30-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: اللَّطِيف ›
moon-icon

Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

  • Muharram
    image
    مُحَرَّمْ
  • Swafar
    image
    صَفَرْ
  • Rabiy’u Al-Awwal
    Rabiy’u Al-Awwal
    رَبيعُ الْأَوًّلْ
  • Rabiy'u Al-Aakhir
    Rabiy'u Al-Aakhir
    رَبيعُ الآخِرْ
  • Jumaadaa Al-Uwlaa
    image
    جُمَادَى الْأُوْلَى
  • Jumaadaa Al-Aakhirah
    image
    جُمَادَى الْآخِرَة
  • Rajab
    image
    رَجَبْ
  • Sha'baan
    Shabaan
    شَعْبَانْ
  • Ramadhwaan
    iocn
    رَمَضَانْ
  • Shawwaal
    image
    شَوّالْ
  • Dhul-Qa’dah
    image
    ذُو الْقَعْدَةْ
  • Dhul-Hijjah
    icon
    ذُو الحِجَّةْ
Alhidaaya.com homepage
  • Kuhusu Alhidaaya
  • Maoni Yako-Wasiliana Na sisi (Contact Us)
  • Tovuti Muhimu

© 2026 Alhidaaya.com All rights reserved.