Skip to main content

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تلقين المحتضر : لا إله إِلاَّ اللهُ

07-Mlango Wa Kumlakinia Anayekata Roho kwa Kalima "Laa ILaaha Illa Allaah"

Alhidaaya.com

Hadiyth – 1

عن معاذ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ كَانَ آخِرَ كَلامِهِ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ دَخَلَ الجَنَّةَ )) رواه أَبُو داود والحاكم ، وقال : (( صحيح الإسناد )) .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote yatakayokua maneno yake ya mwisho Laa ilaaha illa Allaah (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Allaah) ataingiya peponi." [Abuu Daawuwd na Al-Haakim, na akasema Isnaad yake ni Swahiyh]

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Walakinieni mauti wenu kwa neno, Laa ilaaha illa Allaah." [Muslim]