21-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Kufiwa na Watoto Wachanga

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل من مات لَهُ أولاد صغار

21-Mlango Wa Ubora wa Kufiwa na Watoto Wachanga

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَمُوتُ لَهُ ثَلاَثَةٌ لَمْ يَبْلُغوا الحِنْثَ إِلاَّ أدْخَلَهُ اللهُ الجَنَّةَ بِفَضْلِ رَحْمَتِهِ إيَّاهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna Muislamu yeyote anayefiwa na watoto watatu ambao hawaja baleghe isipokuwa Allaah atamuingiza Peponi kwa fadhila ya rehma Yake kwao (yaani watoto)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَمُوتُ لأَحَدٍ مِنَ المُسْلِمينَ ثَلاَثَةٌ مِنَ الوَلَدِ لاَ تَمسُّهُ النَّارُ إِلاَّ تَحِلَّةَ القَسَمِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Moto hautamgusa Muislamu aliyefiwa na watoto watatu ila hadiya kwa kutekeleza yamini." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، قَالَ : جَاءتِ امْرأةٌ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَتْ : يَا رسولَ الله ، ذَهبَ الرِّجَالُ بِحَدِيثكَ ، فَاجْعَلْ لَنَا مِنْ نَفْسِكَ يَوْماً نَأتِيكَ فِيهِ تُعَلِّمُنَا مِمَّا عَلَّمَكَ اللهُ ، قَالَ : (( اجْتَمِعْنَ يَوْمَ كَذَا وَكَذَا )) فَاجْتَمَعْنَ ، فَأَتَاهُنَّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَّمَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَهُ اللهُ ، ثُمَّ قَالَ : (( مَا مِنْكُنَّ مِنِ امْرَأةٍ تُقَدِّمُ ثَلاَثَةً مِنَ الوَلَدِ إِلاَّ كَانُوا لَهَا حِجَاباً مِنَ النَّارِ )) فقالتِ امْرَأةٌ : وَاثْنَينِ ؟ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( وَاثْنَيْنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Sa'iyd Al-Khudriy: mwanamke Alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume wametutangulia kwa Hadiyth zako, hivyo tuwekee siku ambayo tutakuja kwako ili utufundishe aliyo kufundisha Allaah." Akasema: "Kusanyikeni siku kadha wa kadha." Wanawake wakakusanyika siku iliyopangwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja kwao na kuwafundisha aliyofunuliwa na Allaah, kisha akasema: "Hakuna yeyote miongoni mwenu ambaye atawatanguliza (atafiwa) watoto watatu isipokuwa watakuwa ni kinga kwake na Moto." Mwanamke mmoja Akasema: "je, na wawili?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na wawili pia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share