22-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kulia Kuwa na Hofu Wakati wa Kupita Kwenye Makaburi ya Madhalimu, Kunyenyekea kwa Allaah na Onyo kwa Kughafilika na Hilo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب البكاء والخوف عِنْدَ المرور بقبور الظالمين

ومصارعهم وإظهار الافتقار إِلَى الله تَعَالَى

والتحذير من الغفلة عن ذلك

22-Mlango Wa Kulia Kuwa na Hofu Wakati wa Kupita Kwenye Makaburi ya Madhalimu, Kunyenyekea kwa Allaah na Onyo kwa Kughafilika na Hilo

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عن ابن عمرَ رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ لأصْحَابِهِ - يعْني لَمَّا وَصَلُوا الحِجْرَ - دِيَارَ ثَمُودَ - : (( لاَ تَدْخُلُوا عَلَى هَؤُلاَءِ المُعَذَّبِينَ إِلاَّ أنْ تَكُونُوا بَاكِينَ ، فَإنْ لَمْ تَكُونُوا بَاكِينَ ، فَلاَ تَدْخُلُوا عَلَيْهِمْ ، لاَ يُصِيبُكُمْ مَا أصَابَهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ قَالَ : لَمَّا مَرَّ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِالحِجْرِ ، قَالَ : (( لاَ تَدْخُلُوا مَسَاكِنَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أنْفُسَهُمْ ، أنْ يُصِيبَكُمْ مَا أصَابَهُمْ ، إِلاَّ أنْ تَكُونُوا بَاكِينَ )) ثُمَّ قَنَّع رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، رَأسَهُ وأسْرَعَ السَّيْرَ حَتَّى أجَازَ الوَادِي .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia Sahaaba zake (yaani walipowasili Hijr), nyumba na ardhi ya Thamuwd: "Musiingie kwa hawa watu wanaoadhibiwa isipokuwa mkiwa mnalia (kwa kuonyesha huzuni na hofu); Ikiwa hamtalia, basi musiingie kabisa katika sehemu hiyo musije mukafikiwa na yale yaliowakumba wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyingine amesema: Alipopita Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hijr alisema: "Musiingie katika makazi ya wale waliodhulumu nafsi zao ili musifikiwe na yale yalio wafika ila ikiwa mtakuwa ni wenye kulia." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alijifunika kichwa chake kwa nguo na akakaza mwendo hadi akapita bonde hilo.

 

 

 

Share