Skip to main content

08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Fadhila Mbalimbali - كِتابُ الْفَضائِل34-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuswali Swalaah ya Ramadhwaan Nayo ni Tarawehe

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب استحباب قيام رمضان وَهُوَ التراويح

34-Mlango Wa Kupendeza Kuswali Swalaah ya Ramadhwaan Nayo ni Tarawehe

Alhidaaya.com

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إيماناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhwaan kwa 'Ibadah hali ya kuwa na Imaani, na hali ya kutarajia kupata thawabu mtu huyo husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُرَغِّبُ في قِيَامِ رَمَضَانَ مِنْ غَيْرِ أنْ يَأمُرَهُمْ فِيهِ بِعَزِيمَةٍ ، فيقولُ : (( مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إيمَاناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) رواه مسلم .

Na amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) : Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akihimiza kusimamisha usiku wa Ramadhwaan bila kuwaamuru wao kuwa ni lazima akisema: "Mwenye kusimama usiku Ramadhwaan kwa Imaani, na kutarajia thawabu huyo husamehewa madhambi yake yaliyotangulia." [Muslim]