Skip to main content

09A-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume012-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

Alhidaaya.com 

012-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa:  Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali:

Ni kama simba, chui, duma na kadhalika.  Ni haramu kuvaa nguo au viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi za wanyama hawa kutokana na neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa  aalihi wa sallam):

"لَا تَرْكَبُوا الْخَزَّ وَلَا النِّمَارَ"

“Msikalie hariri wala ngozi ya chui”[Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4129) na Ibn Maajah (3656)].

Rasuli amekataza kutumia vitu hivi kutokana na kuwa ni mapambo, na kuwa vinajenga kiburi kwa mtumiaji, lakini pia ni nguo za watu wasio na asili ya Uarabu (Waajemi).  [‘Awnul Ma’abuwd (11/188)]