Skip to main content

10B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا Posa Na Hukumu Zake17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Kama Mwanaume Hajapendezwa Na Mwanamke, Nini Afanye?

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

Posa Na Hukumu Zake

Alhidaaya.com

17:   Kama Mwanaume Hajapendezwa Na Mwanamke, Nini Afanye?

Kama mwanaume atamwangalia mwanamke na asimpendeze, basi analotakiwa ni kunyamaza.  Haifai kutangazia chochote cha kumchafua mwanamke au familia yake.  Yale ambayo hayakumpendeza yeye yanaweza yakamfurahisha mwingine.  Ni vizuri pia asiseme kwamba hamtaki, hilo linaumiza, anyamaze tu.