Skip to main content

Majini05-Majini: Mada Waliyoumbiwa Kwayo Majini

Majini

Alhidaaya.com 

05-  Mada Waliyoumbiwa Kwayo Majini:

Majini wameumbwa kutokana na moto.  Allaah Ta’aalaa Anasema:

"وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ"

Na majini Tuliwaumba kabla kutokana na moto ulio mkali mno”.  [Al-Hijri:  27]

Ayah hii ni dalili pia kwamba majini waliumbwa kabla ya sisi wanadamu.

Allaah Anasema tena:  

"وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ"

Na Akaumba majini kutokana na mwako wa moto”.  [Ar-Rahmaan:  15]

Ash-Shawkaaniy amesema:  “Allaah Amemuumba Al-Jaann kutokana na moto, na Al-Jaann ndiye baba wa majini.  Na المارِجُ ni mwako safi wa moto usio na moshi.

Na Amesema tena Allaah Ta’aalaa:

"قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ"

“(Allaah) Akasema:  Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha?  (Ibliys) Akasema:  Mimi ni mbora zaidi kuliko yeye.  Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo”.     [Al-A’araaf:  12]

Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) amesema:

"خُلِقَتِ الْمَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ‏"

“Malaika wameumbwa kutokana na nuru, na majini wameumbwa kutokana na mwako mchanganyo wa moto, na Aadam ameumbwa kutokana na hicho mlichoelezewa (udongo)”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (2996)]