Skip to main content

10E-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الصَّدَاقُ: Mahari08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake: Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili (b) Mke Akikaa Mwaka Mzima Kwenye Nyumba Ya Mumewe Hata Bila Ya Kuingiliwa

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الصَّدَاقُ

Mahari

Alhidaaya.com

08:  Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake: Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili (b) Mke Akikaa Mwaka Mzima Kwenye Nyumba Ya Mumewe Hata Bila Ya Kuingiliwa:

Kwa mujibu wa kauli ya Wamaalik, ikiwa mtu ameoa mke, na mke akapelekwa kwake, halafu akakaa kwake mwaka mzima bila kumuingilia, basi ni lazima atoe mahari kamili kwa mujibu wa Wamaalik.

Ninasema:  “Sioni dalili yoyote kuhusiana na wao kuainisha kipindi cha mwaka mmoja.  Lau mwanamke atapelekwa kwa mumewe, na akakaa bila kumuingilia, hili litarejeshwa kwenye hali iliyotangulia kuelezwa (faragha sahihi inayozingatiwa).  Yaliyoelezwa huko ndiyo yatakayosemwa kuhusiana na hili”.