Skip to main content

10E-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الصَّدَاقُ: Mahari13-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Ikiwa Zitatajwa Mahari Mbili

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الصَّدَاقُ

Mahari

Alhidaaya.com

13:   Ikiwa Zitatajwa Mahari Mbili:

Ikiwa watu wa mke watamtaka mume ataje mahari mbili; moja kwa ajili ya ‘aqdi, na nyingine kwa ajili ya kutangazwa hadhirani kwa lengo la kujifaharishia kwa watu na si kwamba ndio inayomlazimu kutoa, hapa Jumhuwr ya ‘Ulamaa -kinyume na Mahanbali- wanasema kwamba atatoa iliyobainishwa kwenye ‘aqdi, na si ile iliyotangazwa mbele za watu.  Ni chaguo pia la Sheikh wa Uislamu.