Skip to main content

10K-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: النُّشُوْزُ وَعِلَاجُهُ Uasi Wa Mke Kwa Mume Na Njia Za Kuutibu01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Uasi Wa Mke Kwa Mume Na Njia Za Kuutibu: Maana Ya An-Nushuwz: Uasi Wa Mke

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa 

النُّشُوْزُ وَعِلَاجُهُ

Uasi Wa Mke Kwa Mume Na Njia Za Kuutibu

Alhidaaya.com 

01:  MaanaYa "النُّشُوزُ": An-Nushuwz

"النُّشُوزُ" ni neno lililotokana na  "النَّشْزُ", na maana yake ni mahali paliponyanyuka.  Ama kiistilahi, ni mke kumwasi mumewe akaacha utiifu ambao Allaah Amemfaradhishia.  Inakuwa kama vile amejiweka juu yake badala ya chini yake.

Jambo hili ni haramu, kwa kuwa Allaah Ta'alaa Amempangia mume adhabu ya kumpa mkewe mwasi kama hatokoma kwa njia ya kumnasihi kwa maneno, na adhabu haiwi ila kwa kufanya la haramu au kuacha la wajibu. Allaah Amesema:

"وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا"

"Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru).  Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi).  Hakika Allaah daima Ni Mwenye Uluwa, Mkubwa wa Dhati, Vitendo na Sifa".  [An-Nisaa: 34]