Skip to main content
Majina Mazuri Ya Allaah Jina 001 kati ya 103
Allaah — Majina Mazuri ya Allaah

Allaah: Mwenye Uluwhiyyah; Muabudiwa wa Haki Pekee

Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwenye Uluwhiyyah (Anayestahiki kuabudiwa Pekee bila kushirikishwa na yeyote), na Ndiye Mwenye kustahiki Al-‘Ubuwdiyyah kutoka kwa viumbe Vyake wote; nayo ni unyenyekevu, mapenzi, khofu ya Adhabu Yake na kutaraji Rehma Yake, utiifu na kujidhalilisha mbele Yake, kutovuka Mipaka Yake, kutekeleza Maamrisho Yake na kujiepusha na Makatazo Yake, kwa ajili ya kujikurubisha Kwake, kutaka Thawabu Zake na kujihadhari na Ghadhabu Yake na Ikabu Yake.

Yeye Ndiye Mwenye kustahiki kupwekeshwa katika ‘ibaadah kwa Alivyojisifu Mwenyewe kwa Sifa za Uluwhiyyah, nazo ni Sifa za ukamilifu. Na Yeye Ndiye Mwenye kustahiki kuelekewa kwa mapenzi, unyenyekevu, khofu, matumaini, matarajio, kuadhimishwa na kutiiwa.

Jina hili tukufu la ‘Allaah’ limetajwa katika Qur-aan mara 2699 (elfu mbili, mia sita na tisini na tisa), na ndilo neno lililotajwa kwa wingi zaidi katika Qur-aan nzima. Miongoni mwa Aayaat hizo ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu). Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya Idhini Yake? Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu Ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Taadhima. [Al-Baqarah (2:255)]

Na Anasema pia (سبحانه وتعالى):

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa. [Twaahaa (20:8)]

Maana Ya Jina La Allaah Kilugha:

Asili ya Jina ‘Allaah’ ni ‘Al-Ilaah’ (الإِلَٰه), na Al-Ilaah katika lugha ya Kiarabu ina maana nne:

Kwanza: Al-Ma’buwd; Mwenye kuabudiwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾

Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. [Az-Zukhruf (43:84)]

Pili: Mwenye kukimbiliwa katika hali ya khofu na shida. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾

Na wamejichukulia badala ya Allaah waabudiwa ili wakitumaini kuwa watanusuriwa! [Yaasiyn (36:74)]

Yaani: Wanataraji wawanusuru dhidi ya maadui wao; na Waarabu walikuwa wakiielekea miungu yao kuiomba nusura.

Tatu: Al-Mahbuwb Al-Mu’adhwam; Mpendwa, Mtukuzwa. Waarabu walikuwa wakiyapenda masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu na wakiyatukuza. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

Na miongoni mwa watu wako wenye kuwafanya viumbe miungu badala ya Allaah, wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wale waliodhulumu wangelitambua watakapoona adhabu, kwamba nguvu zote ni za Allaah, na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa Kuadhibu, (basi wasingelimfanyia Allaah washirika). [Al-Baqarah (2:165)]

Nne: Ambaye akili hukanganyika katika kumtafakari; yaani nyoyo hukanganyika zinapotafakari Utukufu Wake (سبحانه وتعالى), kisha zikashindwa kufikia kuijua hakika ya Dhati Yake, Ujalali Wake na Utukufu Wake (عزّ وجلّ).

Jina hili ndilo Jina tukufu kabisa miongoni mwa Al-Asmaa Al-Husnaa, lililotukuka zaidi na lililojumuisha maana za Majina Yake yote. Allaah (تبارك وتعالى) Amejihusisha Nalo Pekee kutokana na walimwengu wote, hata washirikina walilitambua, na ndimi zao zikalitamka bila kipingamizi wala kusita pale walipoulizwa kuhusu Muumbaji. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Allaah. Sema: AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah). Bali wengi wao hawajui. [Luqmaan (31:25)]

Sifa Mahsusi Za Jina Hili Tukufu La Allaah:

Jina hili tukufu lina sifa mahsusi zisizokuwa katika Jina lingine lolote miongoni mwa Majina Yake, nazo ni:1

1-Ni Jina mahsusi (عَلَم) la Dhati ya Allaah (سبحانه وتعالى), si kama Majina mengine ambayo yamenyambuliwa kutokana na Sifa na vitendo, kama Ar-Rahmaan (kutokana na Rehma) na Al-Khaaliq (kutokana na uumbaji). Na ‘Ulamaa wamekhitilafiana kama Jina hili limenyambuliwa kutokana na Al-Ilaah (kama ilivyotajwa juu) au la; na vyovyote iwavyo, Jina hili linabeba maana ya Uluwhiyyah (kustahiki kuabudiwa) Aliyojihusisha nayo Allaah Pekee.

2-Ni Jina ambalo hakuitwa kwalo yeyote isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى); Allaah Amezizuia ndimi za viumbe kuitwa kwalo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)? [Maryam (19:65)]

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Hakuna yeyote anayeitwa Ar-Rahmaan isipokuwa Allaah (تبارك وتعالى).2 Basi hali kadhaalika hakuna anayeitwa Allaah isipokuwa Yeye (سبحانه وتعالى) Pekee.

3-Ni asili ya Majina Yake yote, na Majina mengine yote yanaegemezwa Kwake. Husemwa: Ar-Rahmaan, Ar-Rahiym, Al-Qudduws, As-Salaam, Al-‘Aziyz na Al-Hakiym ni miongoni mwa Majina ya Allaah; wala haisemwi: Allaah ni miongoni mwa Majina ya Ar-Rahmaan, au ni miongoni mwa Majina ya Al-‘Aziyz. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf (7:180)]

Na Anasema (سبحانه وتعالى):

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾

Yeye Ni Allaah, Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ya ghaibu na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu. [Al-Hashr (59:22)]

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye Kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye Kusadikisha ahadi na Kuaminisha, Mwenye Kudhibiti Kushuhudia Kuchunga na Kuhifadhi, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Jabari Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye Ukubwa na Uadhama, Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha. [Al-Hashr (59:23)]

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi wa viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa. Kinamsabihi Pekee kila kilichoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Hashr (59:24)]

4-Ni Jina linalojumuisha Majina Mazuri yote na Sifa tukufu zote za Allaah (سبحانه وتعالى). Na ndio maana mja anapoomba akasema: اللَّهُمَّ, huwa amemwomba Allaah kwa Majina Yake Mazuri yote na Sifa Zake tukufu.3 Na herufi ya (م) katika اللَّهُمَّ imewekwa badala ya herufi ya kuita (يَا), kwa hiyo haisemwi: يَا اللَّهُمَّ. Al-Hasan Al-Baswriy amesema: اللَّهُمَّ ni mjumuiko wa du’aa. Na An-Nadhwr bin Shumayl amesema: Mwenye kusema: اللَّهُمَّ, basi amemwomba Allaah kwa Majina Yake yote. Na ndio maana baadhi ya ‘Ulamaa wakaona kuwa Jina hili la Allaah Ndilo Jina tukufu kabisa (الاسْمُ الأَعْظَم) ambalo Akiombwa kwalo du’aa Huitikia. Rejea chini: Nukta ya (13) katika Taathira ya imaan.

5-Herufi mbili za mwanzo (ال) ni sehemu ya asili ya Jina hili, na hazikuingia kwa ajili ya kulifanya kuwa maalumu. Dalili yake ni kwamba hazidondoki pale linapotanguliwa na herufi ya kuita; husemwa: يَا اللَّه, ilhali katika Majina mengine hazibaki; husemwa: يَا رَحْمَٰن, wala haisemwi: يَا الرَّحْمَٰن. Na imesemwa pia kwamba kutodondoka kwake ni dalili kwamba kulijua Jina hili ni kwa daima, halitoweki.

6-Ni Jina la kwanza katika Aayah ya kwanza ya Qur-aan:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu). [Al-Faatihah (1:1)]

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki) Allaah Rabb wa walimwengu. [Al-Faatihah (1:2)]

Na katika Suwrah ya mwisho ya Qur-aan limetajwa neno Ilaah ambalo ndilo asili ya Jina hili:

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾

Sema: Najikinga na Rabb wa watu. Mfalme wa watu. Muabudiwa wa Haki wa watu. [An-Naas (114:1-3)]

7-Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyahusisha kwa kuyataja Majina mawili; Allaah na Ar-Rahmaan, katika Kauli Yake:

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa (17:110)]

Ameyahusisha hivyo kwa sababu ya utukufu wa Majina hayo mawili, na Jina la ‘Allaah’ ni tukufu zaidi, kwani limetangulizwa kabla ya Ar-Rahmaan.

8-Kalimah ya Shahaadah ambayo kwayo mtu huingia katika Uislamu kutoka katika ukafiri, haikutajwa ndani yake isipokuwa Jina hili:

أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ

Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah.

Na haisihi shahaadah kwa kusema: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا الْقُدُّوس au kwa Jina lingine lolote isipokuwa Jina la Allaah. Na Allaah Mwenyewe Ameshuhudia hilo:

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na (pia) Malaika na wenye ilimu wameshuhudia hilo. Na Yeye mbali ya hilo, Anasifika kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan (3:18)]

9-Kwa utukufu wake, Allaah Atalinyanyua kutoka ardhini mwishoni mwa zama, pale Atakapozichukua roho za Waumini. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ عَلَى أَحَدٍ يَقُولُ: اللَّهُ اللَّهُ))

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Saa (Qiyaamah) haitosimama juu ya mtu yeyote anayesema: Allaah, Allaah.” [Muslim]

10-Jina hili limehusishwa na Adhaan na Takbiyr ya Swalaah. Adhaan huanza kwa Jina la Allaah na huishia kwa Jina la Allaah, na neno la kwanza la Swalaah ni اللَّهُ أَكْبَرُ, na Jina hili ndilo linalotajwa zaidi kuliko maneno mengine katika Swalaah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنْ عَلِيٍّ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((مِفْتَاحُ الصَّلاَةِ الطُّهُورُ، وَتَحْرِيمُهَا التَّكْبِيرُ، وَتَحْلِيلُهَا التَّسْلِيمُ))

Amesimulia ‘Aliy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ufunguo wa Swalaah ni twahara, na kuharamisha kwake (yasiyofaa ndani yake) ni Takbiyr, na kuhalalisha kwake ni Tasliym.” [Abuu Daawuwd (61), At-Tirmidhiy (3), Ibn Maajah (275); na Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha riwaayah ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه) yenye maneno haya katika Swahiyh At-Tirmidhiy (238)]

11-Jina hili limehusishwa katika viapo kwa namna isiyokuwa kwa Majina mengine, kama kusema: تَاللَّهِ na وَايْمُ اللَّهِ.

Taathira Ya Imaan, Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah:

1-Mpwekeshe Allaah Katika ‘Ibaadah Zako Zote:

Tambua kwamba Allaah Ndiye Pekee Mwenye maana zote za Uluwhiyyah, basi usimwelekee mwengine yeyote katika ‘ibaadah yoyote; si kwa du’aa, wala kwa kuchinja, wala kwa nadhiri, wala kwa kutaka msaada katika yasiyowezwa isipokuwa na Allaah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu. [Al-Baqarah (2:163)]

2-Tambua Kwamba Jina Allaah Ndilo Asili Ya Majina Mengine Yote:

Majina yote Mazuri ya Allaah yanaambatanishwa na Jina hili; husemwa: Ar-Rahmaan ni miongoni mwa Majina ya Allaah, wala haisemwi: Allaah ni miongoni mwa Majina ya Ar-Rahmaan. Tazama jinsi Majina yote yanavyofuata baada ya Jina hili tukufu: Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾ هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾ هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾

Yeye Ni Allaah, Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ya ghaibu na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu. Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye Kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye Kusadikisha ahadi na Kuaminisha, Mwenye Kudhibiti Kushuhudia Kuchunga na Kuhifadhi, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Jabari Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye Ukubwa na Uadhama, Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha. Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi wa viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa. Kinamsabihi Pekee kila kilichoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Hashr (59:22-24)]

3-Hakuna Yeyote Aliyeitwa Kwa Jina Hili Isipokuwa Yeye:

Jina Allaah ni mahsusi Kwake (سبحانه وتعالى); hakuna kiumbe aliyepewa jina hili, wala hakuna anayelingana Naye katika Sifa Zake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)? [Maryam (19:65)]

4-Muombe Allaah Kwa Majina Yake Mazuri Na Jiepushe Na Kuyapotosha:

Katika kumuadhimisha Allaah ni kuyathibitisha Majina Yake kama yalivyokuja, bila kuyapotosha maana yake, wala kuwaita viumbe kwayo, wala kumwita kwa majina Asiyojiita. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf (7:180)]

5-Mnyenyekee Allaah Na Ujaze Moyo Wako Haiba Yake Na Kumtukuza:

Muumini anapolitafakari Jina la Allaah akatambua kwamba Yeye Pekee Ndiye Mwenye kuabudiwa, humnyenyekea, humkhushuu, na huulazimisha moyo wake kumkhofu na kumtukuza. Na hiyo ndiyo sifa ya Waumini wa kweli. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٢﴾

Hakika Waumini ni wale ambao Anapotajwa Allaah, nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia imaan, na kwa Rabb wao wanatawakali. [Al-Anfaal (8:2)]

6-Mpende Allaah Kuliko Vyote, Umkhofu Na Umtarajie:

Kumbuka kwamba moyo wa Muumini unapaswa kufungamana na Rabb wake kwa mapenzi, khofu na matarajio. Na mapenzi ya Waumini kwa Allaah ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya washirikina kwa miungu yao (Rejea juu: Al-Baqarah (2:165)). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) عَنِ النَّبِيِّ (صلى الله عليه وسلم) قَالَ: ((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ، وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ))

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa imaan: Allaah na Rasuli Wake wawe wapenzi zaidi kwake kuliko wengineo wote, ampende mtu hampendi isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri kama anavyochukia kutupwa motoni.” [Al-Bukhaariy] [Muslim]

7-Rejea Kwa Allaah Katika Mambo Yako Yote Na Usiwategemee Viumbe:

Tambua kwamba viumbe hawana hila wala nguvu isipokuwa kwa Allaah, basi elekeza moyo wako Kwake katika kila jambo lako, na uache kuwategemea viumbe. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: كُنْتُ خَلْفَ رَسُولِ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) يَوْمًا فَقَالَ: ((يَا غُلاَمُ، إِنِّي أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللَّهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللَّهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلِ اللَّهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ ...))

Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Yaa kijana! Hakika mimi nakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah (kwa kufuata Amri Zake) Atakuhifadhi; mhifadhi Allaah utamkuta mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah, na unapotaka msaada, taka msaada kwa Allaah ...” [At-Tirmidhiy (2516), na Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh At-Tirmidhiy]

8-Kithirisha Kumdhukuru Allaah Katika Kila Hali:

Fungamanisha kila wakati wa maisha yako na Jina la Allaah; kwa kuanza mambo yako kwa بِسْمِ اللَّهِ, kumshukuru kwa الْحَمْدُ لِلَّهِ, na kumtukuza kwa اللَّهُ أَكْبَرُ. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾

Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru. [Al-Baqarah (2:152)]

9-Anza Mambo Yako Kwa Jina La Allaah:

Muumini huanza mambo yake kwa Jina la Allaah, akitafuta baraka na Msaada Wake, kama alivyofundisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

عَنْ عُمَرَ بْنِ أَبِي سَلَمَةَ (رضي الله عنهما) قَالَ: كُنْتُ غُلاَمًا فِي حَجْرِ رَسُولِ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم)، وَكَانَتْ يَدِي تَطِيشُ فِي الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((يَا غُلاَمُ، سَمِّ اللَّهَ، وَكُلْ بِيَمِينِكَ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ))

Amesimulia ‘Umar bin Abiy Salamah (رضي الله عنهما): Nilikuwa kijana chini ya malezi ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na mkono wangu ulikuwa ukizunguka kila upande katika sahani. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: “Yaa kijana! Taja Jina la Allaah (sema: بِسْمِ اللَّهِ), na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kilicho karibu nawe.” [Al-Bukhaariy] [Muslim]

10-Liadhimishe Jina La Allaah: Usiape Isipokuwa Kwa Allaah:

Katika kuliadhimisha Jina la Allaah ni kutoapa isipokuwa kwa Allaah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنِ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) قَالَ: ((أَلاَ إِنَّ اللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ، مَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أَوْ لِيَصْمُتْ))

Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Tanabahi! Hakika Allaah Anakukatazeni kuapa kwa baba zenu. Anayetaka kuapa, basi aape kwa Allaah au anyamaze.” [Al-Bukhaariy] [Muslim]

11-Wape Watoto Wako Majina Ya ‘Abdullaah Na ‘Abdur-Rahmaan:

Miongoni mwa khaswa za Jina hili ni kwamba majina yanayopendwa zaidi na Allaah ni yale yanayoonyesha uja Kwake. Basi wachagulie watoto wako majina hayo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنِ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((إِنَّ أَحَبَّ أَسْمَائِكُمْ إِلَى اللَّهِ عَبْدُ اللَّهِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ))

Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika majina yenu yanayopendwa zaidi na Allaah ni ‘Abdullaah na ‘Abdur-Rahmaan.” [Muslim]

12-Jitahidi Maneno Yako Ya Mwisho Duniani Yawe: لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ:

Kama ulivyoishi na Jina la Allaah katika Adhaan zako, Swalaah zako na dhikr zako, basi jitahidi mwisho wa maisha yako uwe kwa kulitaja Jina hili tukufu, kwa kudumisha Tawhiyd na dhikr katika maisha yako yote. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((مَنْ كَانَ آخِرُ كَلاَمِهِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ))

Amesimulia Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ

Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ataingia Jannah.” [Abuu Daawuwd (3116), na Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Abiy Daawuwd]

13-Muombe Allaah Kwa Jina Lake Hili Tukufu Na Kwa Majina Yake Mazuri:

Omba Du’aa kwa kutanguliza Jina la Allaah na Majina Yake Mazuri kama Alivyoamrisha (Rejea juu: Al-A’raaf (7:180)), kwani kumwomba kwa Majina Yake ni katika sababu kubwa za kutakabaliwa du’aa.

عَنْ بُرَيْدَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) سَمِعَ رَجُلاً يَقُولُ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الأَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ. فَقَالَ: ((لَقَدْ سَأَلْتَ اللَّهَ بِالاِسْمِ الَّذِي إِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى وَإِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ))

Amesimulia Buraydah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsikia mtu akisema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الأَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ

Yaa Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa kuwa nashuhudia kwamba Wewe Ndiye Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Al-Ahad (Mmoja Pekee), Asw-Swamad (Mkusudiwa wa haja zote), Ambaye Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.

Akasema: “Kwa yakini umemwomba Allaah kwa Jina Ambalo Akiombwa kwalo Hutoa, na Akiombwa du’aa kwalo Huitikia.” [Abuu Daawuwd (1493), At-Tirmidhiy (3475), Ibn Maajah (3857); At-Tirmidhiy amesema: Hasan Ghariyb]

Na Allaah Mjuzi zaidi

  • 1Imenukuliwa kwa mabadiliko na nyongeza kutoka kwa An-Najdiy, naye amenukuu kutoka kwa Fakhrud-Diyn Ar-Raaziy.
  • 2Tafsiyr Ibn Kathiyr.
  • 3Madaarij As-Saalikiyn (1/32).