Skip to main content
Majina Mazuri Ya Allaah Jina 083 kati ya 103
Al-Waasi' — Majina Mazuri ya Allaah

Al-Waasi’: Mwenye wasaa; Ambaye Sifa Zake ni pana zisizo na mipaka: Ujuzi Wake, Rehma Yake, Maghfirah Yake na Fadhila Zake zimeenea kila kitu.

Jina hili tukufu limetajwa katika Qur-aan mara tisa, na mara nyingi limeambatana na Jina Al-‘Aliym. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah. Basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah (2:115)]

Na Anasema pia:

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah (2:261)]

Maana Ya Al-Waasi’:

1-Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mwenye wasaa katika Dhati Yake na Sifa Zake; hakuna kinachoweza kumzunguka, na Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayatul-Kursiy:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu). Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya Idhini Yake? Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu Ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Taadhima. [Al-Baqarah (2:255)]

2-Rehma Yake imekienea kila kitu, na Ujuzi Wake umekizunguka kila kitu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾

(Malaika) ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih na kumhimidi Rabb wao, na wanamwamini, na wanawaombea maghfirah wale walioamini (wakisema): Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa Rehma na ujuzi, basi Waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na Wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno. [Ghaafir (40:7)]

3-Maghfirah Yake ni pana kwa wanaojiepusha na madhambi makubwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogo-madogo. Hakika Rabb wako Ni Mkunjufu wa Kughufuria. Yeye Anakujueni vyema, tangu Alipokuanzisheni kutoka katika ardhi, na pale mlipokuwa mimba changa matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm (53:32)]

4-Fadhila Zake na rizki Yake ni pana; Anamtajirisha Amtakaye. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٢﴾

Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha katika Fadhila Zake. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [An-Nuwr (24:32)]

Taathira Ya Imaan, Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah, Al-Waasi’:

1-Usikate Tamaa Na Rehma Ya Al-Waasi’:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Waasi’, kwamba Rehma ya Allaah imeenea kila kitu, na Ameiandika kwa namna maalumu kwa wenye taqwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. (Allaah) Akasema: Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rehma Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) Zetu. [Al-A’raaf (7:156)]

2-Kimbilia Maghfirah Pana Ya Al-Waasi’:

Tambua, ee Mja wa Al-Waasi’, kwamba Maghfirah Yake ni pana kuliko madhambi yako (rejea An-Najm (53:32) juu); basi usiache kutubia.

3-Usiogope Ufakiri Unapooa, Kwani Al-Waasi’ Atakutajirisha:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Waasi’, kwamba Allaah Ameahidi kuwatajirisha mafakiri wanaooa kwa ajili ya kujistahi (rejea An-Nuwr (24:32) juu).

4-Ikiwa Mke Na Mume Wametengana, Al-Waasi’ Atamtosheleza Kila Mmoja:

Tambua kwamba hata katika mtengano, Al-Waasi’ Anaahidi kumtosheleza kila mmoja kutokana na wasaa Wake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴿١٣٠﴾

Na wakifarikiana basi Allaah Atamtosheleza kila mmoja kwa Wasaa Wake. Na Allaah daima Ni Mwenye Wasaa, Mwenye Hikmah wa yote. [An-Nisaa (4:130)]

5-Toa Katika Njia Ya Allaah, Kwani Al-Waasi’ Huzidisha:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Waasi’, kwamba swadaqah moja huzidishwa mara mia saba au zaidi (rejea Al-Baqarah (2:261) juu).

6-Usifuate Vitisho Vya Shaytwaan Vya Ufakiri:

Tahadhari na shaytwaan anayekutisha kwa ufakiri unapotaka kutoa; bali Al-Waasi’ Anakuahidi Maghfirah na Fadhila. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini Maghfirah kutoka Kwake na Fadhila. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah (2:268)]

7-Ardhi Ya Allaah Ni Pana, Basi Mwabudu Popote Ulipo:

Tambua, ee Mja wa Al-Waasi’, kwamba ukizuiwa kumwabudu Allaah mahali fulani, ardhi Yake ni pana. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Enyi Waja Wangu walioamini! Hakika Ardhi Yangu ni pana, basi Mimi Pekee Niabuduni. [Al-‘Ankabuwt (29:56)]

8-Mwelekyaa Allaah Popote Ulipo:

Kumbuka kwamba Mashariki na Magharibi ni za Al-Waasi’ (rejea Al-Baqarah (2:115) juu); basi mwelekee Yeye kwa moyo wako popote utakapokuwa.

9-Wapanulie Watu Kama Al-Waasi’ Anavyokupanulia:

Tambua kwamba anayempa mwenye dhiki muda au kumwepesishia, Al-Waasi’ Humwepesishia duniani na Aakhirah (rejea Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) katika 023-Al-Jabbaar) [Muslim].

10-Mwombe Al-Waasi’ Katika Fadhila Zake Unapotoka Msikitini:

Omba du’aa, ee Mja wa Al-Waasi’, kama alivyofundisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ أَوْ عَنْ أَبِي أُسَيْدٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم): ((إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ))

Amesimulia Abuu Humayd au Abuu Usayd (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mmoja wenu anapoingia Msikitini aseme:

اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ

Yaa Allaah, Nifungulie milango ya Rehma Zako. Na anapotoka aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ

Yaa Allaah, hakika mimi nakuomba katika Fadhila Zako.” [Muslim]

Na Allaah Mjuzi zaidi