|
000-Utangulizi Wa Mhariri
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu).
ضبط نصوصه وخرّج أحاديثه: حلمي بن إسماعيل الرشيدي
Amehakiki matini zake na kutakhrij Hadiyth zake: Hilmiy bin Ismaa‘iyl Ar-Rashiydiy
مقدمة المحقق
Utangulizi Wa Mhariri
إن الحمد لله تعالى نحمده، ونستعين به ونستغفره، ونعوذ بالله تعالى من شرور أنفسنا، وسيئات أعمالنا. ومن يهد الله تعالى فلا مضل له. ومن يضلل فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله.
Hakika Himdi zote ni za Allaah (تعالى); tunamhimidi, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah. Na tunajikinga kwa Allaah (تعالى) kutokana na shari za nafsi zetu na maovu ya amali zetu. Ambaye Allaah (تعالى) Amemwongoa, hakuna wa kumpoteza; na Ambaye Amempoteza, hakuna wa kumwongoa. Na nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, Hana mshirika; na nashuhudia kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.
أما بعد:
Ama baada ya hayo:
فهذا كتاب «٢٠٠ سؤال في العقيدة» للشيخ حافظ أحمد حكمي رحمه الله تعالى، أقدمه لإخواننا الدارسين، وطلاب العلم، وهو مع صغر حجمه، فقد نظمه مؤلفه تنظيماً بديعاً، ورتبه على هيئة سلسلة ملتصقة المبنى والمعنى، جمع فيه أصل الدين وذروة سنامه، وهو التوحيد.
Basi hiki ni kitabu “Maswali 200 Katika ‘Aqiydah” cha Shaykh Haafidhw [bin] Ahmad Hakamiy (رحمه الله تعالى); ninakiwasilisha kwa ndugu zetu wanaosoma na kwa wanafunzi wa ilimu. Nacho, pamoja na udogo wa ukubwa wake, mtunzi wake amekipanga mpangilio wa kupendeza, na amekipangilia kwa sura ya mfululizo unaoshikamana katika muundo wake na maana yake. Amekusanya ndani yake asili ya Dini na kilele cha nundu yake, nayo ni Tawhiyd.
وتأتي أهمية هذا الكتاب، لما حواه بين دفتيه، من عقيدة السلف الذين تربوا عليها وشربوها من رسول الله ﷺ، هذه العقيدة التي لا يُقبل الله تعالى من أحد عقيدة غيرها، فمن أتى الله تعالى بغيرها لا يقبل منه وهو في الآخرة من الخاسرين.
Na umuhimu wa kitabu hiki unatokana na yale kilichoyakusanya baina ya majalada yake mawili, miongoni mwa ‘Aqiydah ya Salaf ambao walilelewa juu yake na wakainywa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). ‘Aqiydah hii ambayo Allaah (تعالى) Hakubali kutoka kwa yeyote ‘aqiydah isiyokuwa hiyo; basi atakayemjia Allaah (تعالى) na isiyokuwa hiyo, haitokubaliwa kutoka kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
والله أسأل أن يكون الكتاب سائقاً بالناس إلى مرضات الله الكريم، مانعاً من ارتكاب الزلات والسيئات والحمد لله على توفيقه، وصلى الله وسلم وبارك على نبينا محمد وعلى آله وصحبه وسلم.
Na Allaah ndiye ninayemuomba Akifanye kitabu hiki kiwe kinachowapeleka watu kwenye Radhi za Allaah Al-Kariym (Mkarimu), na kinachowazuia kutenda makosa na maovu. Na Himdi ni za Allaah kwa Tawfiyq Yake. Na Allaah Amswalie, Amsalimishe na Ambariki Nabiy wetu Muhammad, na ahli zake na Swahaba zake, na Awape amani.