Buns Za Jibini Na Shira

 

  Buns Za Jibini Na Shira

                                      

Vipimo

Unga wa ngano -  3 ½Vikombe visivyojaa

Maziwa -  1 Kikombe

Maji - 1½ Kikombe

Yai - 1

Sukari  -  2 ½Vijiko vya supu

Siagi au mafuta -  ½Kikombe

Hamira - 1 Kijiko cha chai

Chumvi -  ¼Kijiko cha chai

Jibini ya malai (cream cheese) -  Kiasi utakavyotumia kujaza

Shira

Sukari - 2 Vikombe

Maji -  1 ½Vikombe

Zaafarani (iroweke) - ½Kijiko cha chai 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Roweka hamira kwenye maji ya uvuguvugu (warm).
  2. Kisha changanyia vipimo vyote isipokuwa jibini ya malai na shira.
  3. Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini.
  4. Paka siagi kwenye treya ya kuchomea yenye vishimo vidogo.
  5. Halafu fanya viduara vidogo na tia ndani yake jibini ya malai (cream cheese) kwa kutumia kijiko cha chai, na uvifunge viduara vizuri na kuvipanga ndani ya ile treya.
  6. Iwache iimuke (ifure) Kisha ipike kwenye oveni moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 - 25, Kisha washa moto wa juu kidogo tu ili uwive na kugeuka rangi.
  7. Toa katika oveni na mwagia shira na itakuwa tayari kuliwa.
Share