Maana Ya Kauli Ya Allaah (عزَّ وجلَّ): وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ

SWALI:

 

Assalaam Alykum Warahmatullaah Wabarakaatuh! Shukrani zote anastahiki Allah (mwingi wa rehma na mwenye kurehemu) na pia awazidishie kila la khayr katika jihad hii, mie nilikuwa nahitaji fasiri na sherehe ya aya ya mwisho katika surat Wadhuhaa (Fa amma biniy mat rabbika fakhadith)

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu maana ya Aayah. Tafsiri ya Aayah hiyo ni kama ifuatavyo: "Na neema ya Mola wako isimulie" (93: 11).

 

Kwanza hivyo ulivyoandika sivyo, na huwa ni makosa katika kuiandika na kuisoma Qur-aan kwa hali hiyo kwani hubadilisha maana ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Inavyotakiwa kuanzwa Aayah hiyo ni kwa neno ‘Wa' na si 'Fa' kama ulivyoandika. 

Labda huenda tukauliza je, maana ya kuisimulia ni vipi? Jawabu ni kuwa kuisimulia hapa inamaanisha kumshukuru Allaah Aliyetukuka kwa kukupa neema hiyo kwa kufanya amali njema; si kwa njia ya kujisifu. Hakika ni kuwa majisifu kawaida yanampeleka mtu katika kujionyesha (Riyaa), na Riyaa inampeleka mtu kuingia katika Moto wa Jahannam.

 

Na wengine wamefasiri neema hapa kuwa Qur-aan, hivyo akaamrishwa aisome na kuihadithia kwa kuisambaza na kuwafundisha wengine. Nasi pia tunatakiwa tuisome na kuwahadithia mafundisho yake wengine.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share