Mume Kupokea Maiti Ya Mkewe Kaburini Akiwa Ametoka Kwenye Kitendo Cha Ndoa Kabla Ya Kufariki Mkewe

SWALI:

 

 

Asalam Alaykum warahmatulah swali langu linahusu kupokea mayti ndani ya kaburi je mume aliyefiwa na mke anaruhusiwa kupokea maiti hiyo iwapo alishiriki tendo la ndoa na mkewe muda mfupi kabla ya kufa kwa mkewe?

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu mume kupokea maiti ya mkewe kaburini akiwa ametoka katika kitendo cha ndoa.

 

Kwa hakika jambo hilo limekatazwa kama zinavyoonyesha Ahaadiyth zifuatazo:

 

Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kuwa, “Tulikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati bint yake anazikwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anavujwa na machozi yakimiminika kwenye mashavu yake na akauliza, “Je, kuna kati yenu aliyefanya kitendo cha ndoa na mkewe usiku? Abu Twalhah akajibu, “Mimi sikufanya Ee Mjumbe wa Allaah.” Kisha Mtume ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuamrisha ashuke ndani ya kaburi lake (la binti yake Mtume) na kumzika.” [Al-Bukhaariy].

 

Naye Imaam Ahmad katika riwaya nyingine kasimulia wka maneno yaliyo tofauti kidogo hivi: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Mtu aliyefanya tendo la ndoa na mkewe, hapaswi kuingia kwenye kaburi lake.”

 

‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakuingia kwenye kaburi la mkewe.

 

Kwa hiyo wataingia wale Mahaarim wake au watu wowote wengine.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share