Mtoto Wa Kiume Aliyebaleghe Anafaa Kumuosha Baba Yake?

SWALI:

 

ASALAM ALEYKUM,

NAULIZA – MTOTO ALIYEBALEGHE WA KIUME ANARUHUSIWA KUMUOSHA BABA YAKE.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mtoto aliyebaleghe kumuosha baba yake.

 

Hakika ni kuwa ni muhimu zaidi katika kuosha mtu aliyeyekufa awe ni jamaa ya maiti wa karibu. Na ikiwa mtoto yupo basi ni bora zaidi kwani yeye hasa akimuosha mzazi ataweza kuficha aibu ya mzazi wako.

 

Kitu muhimu ambacho kinahitajika kwa huyo mtoto kuweza kuosha mwili wa babake ni kuwa na elimu pamoja na ujuzi wa kufanya kazi hiyo. Ikiwa atakuwa na masharti hayo basi ataruhusiwa na shari’ah bila ya wasiwasi wowote ule.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share