Skip to main content

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah - Imaam Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)002-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Jambo Ambalo Allaah Ameumba Viumbe Kwa Ajili Yake

002-Jambo Ambalo Allaah Ameumba Viumbe Kwa Ajili Yake

Swali:

ما هو ذلك الأمر الذي خلق الله الخلق لأجله؟

Ni lipi jambo hilo ambalo Allaah Ameumba viumbe kwa ajili yake?

Jibu:

قال الله تعالى:

Allaah (تعالى) Amesema:

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ﴿٣٨﴾ مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾

Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa mchezo na upuuzi. Hatukuumba viwili hivyo isipokuwa kwa haki, lakini wengi wao hawajui. [Ad-Dukhaan (44:38-39)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا

Na wala Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake bila kusudio. Hiyo ndio dhana ya wale waliokufuru. [Swaad (38:27)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٢﴾

Na Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili ilipwe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa. [Al-Jaathiyah (45:22)]

وقال تعالى:

Na Amesema (تعالى):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat (51:56)]

الآيات.

Na Aayaat nyinginezo.