Skip to main content

Imaam Al-Albaaniy: Asiolewe Mwanamke Hadi Aache Kufanya Kazi

Asiolewe Mwanamke Mpaka Aache Kufanya Kazi

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

Alhidaaya.com



 

Aliulizwa Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah):

"Je, mwenye kuposa anaweza kumuomba mwanamke ambaye anataka kumposa kuacha kufanya kazi?"



Akajibu:

"Mwenye kuposa hana jukumu hilo juu yake. Hata hivyo, asimuoe ikiwa kama anafanya kazi nje ya nyumba (yake). Haijuzu kwako kumposa na kumuoa ikiwa anafanya kazi nje ya nyumbani kwake."



[Silsilat Al-Hudaa Wa An-Nuwr, kanda namba 174]