Skip to main content

Mukhtasari Wa 'Aqiydah Ya Muislamu: Maswali Na Majibu05-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwanini Allaah Ametuma Rusuli?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 05-Kwanini Allaah Ametuma Rusuli?

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewatuma Rusuli ili walinganie watu kumwabudu na kuepukana na kumshirikisha.

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ

Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.  [An-Nahl: 36]

((الأنبياء إخوةٌ ودينُهُم واحد)) متّفق عَلَيهِ

أَيْ كلُّ الرسل دعوا إِلَى التّوحيد

((Manabiy ni ndugu na Dini yao ni moja)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

Yaani: Rusuli wote wamelingania Tawhiyd