Skip to main content

Fataawaa: Hukmu Mbali Mbali Za Swawm04-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Miji Ambayo Masaa ya kufunga Swawm Ni Marefu Sana

Miji Ambayo Masaa ya kufunga Swawm Ni Marefu Sana

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Tuko katika Mji ambapo jua halizami mpaka saa 3:30 au 4:00 (saa tatu au saa nne) za usiku. Ni lini tunatakiwa tufungue Swawm?

JIBU:

Utafufungua Swawm kufuturu wakati jua linapozama. Maadamu tu mko na mchana na usiku kwa masaa 24, unawajibika kufunga swiyaam, hata kama masaa ni marefu kiasi gani.

[Fataawa Islaamiyah uk. 276, mj. 2]