Kwa Nini Tumswalie Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ?
SWALI:
ASSALAMA ALEYKUM !!!!
NAMSHUKURU ALLA KWA KUTUJAALIA KUIPATA WEBSITE YENYE KUTUNYOOSHA JUU YA DINI YETU. BARAKA ZA ALLA ZIWAENDEE WOTE WENYE KUJIHUSISHA NA 'WEBSITE HII' , KILA MMOJA KWA KIWANGO APENDACHO ALLAH.
SUALI LANGU KWA LEO NI HILI : -
NINI HEKIMA YA KUMSWALIA MTUME. NAHANGAISHWA NA MAWAZO YANGU KWAMBA MTUME NI MJUMBE WA MNWENYEENZI - MUNGU NA AMESHAMTAKASA NA KILA OVU NA AMESHAMWAHIDI PEPO YAKE KILA ZURI YEYE NI KIONGOZI HUKO AKHERA. AMESHATAKASIKA - SASA KWA NINI TUNAHITAJI KUMUOMBEA-OMBEA KILA WAKATI NA WENGINE HATA HATUNA KAULI NJEMA NINI KUMTAJA-TAJA KIPENZI CHA ALLAH. NADHANI SISI NDIO TUKO NJIA PANDA, HATUJIJUI, TUNAHITAJI KUOMBEANA KILA WAKTI.
NAOMBA MAFAHAMISHO. JUU YA HEKIMA ILIYOPO.
A H S A N T E.
JIBU:
بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وعلى آله وصحبه أجمعين و بعد
Kauli yako uliyosema kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ameshatakaswa na maovu na ameshaahidiwa Pepo na kadhalika, na kwamba sisi ndio tunaohitaji kuombeana yote hayo ni kweli kabisa. Lakini bila shaka umetatizwa kufahamu hikma ya kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hivyo Insha Allaah سبحانه وتعالى tutakufahamisha kwa kadiri tunavyoelewa na Allaah سبحانه وتعالى Anajua zaidi.
Anasema Allaah سبحانه وتعالى
((إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا))
((Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake Wanamswalia Nabii. Enyi mlioamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu)) [Al-Ahzaab: 56]
Lakini kwa nini basi tumswalie Mtume صلى الله عليه وآله وسلم? Jibu la swali hakika ni refu
1) Kumtukuza Mtume wa mwisho
Kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni katika kumtukuza kwani yeye ndiye Mtume wa mwisho, na hii ni neema kwetu Umma wa Kiislamu kujaaliwa sisi kuwa yeye ndiye Mtume wetu. Na Allaah سبحانه وتعالى Ametuambia kuwa sisi ni Umma bora kabisa. Bila ya yeye tusingeliweza kupata uongofu kamili (Qur'aan) na mafunzo ya Sunnah ambayo yametutoa kizani na kutuingiza katika nuru.
Na ikiwa Allaah سبحانه وتعالى Mwenyewe Amemtukuza kwa kumtofautisha na mitume mingine yote, kwani wote Amewaita kwa majina
2) Ni ibada kwetu
Kwa vile ni amri kutoka kwa Mola wetu kama tulivyoona katika aya hiyo ya juu, na ndio maana tunamswalia mpaka kwenye Swalah zetu za fardhi na za Sunnah, bila ya kumswalia Swalah haikamiliki.
3) Rahma kwetu kupata fadhila na thawabu zaidi
Binaadamu kila siku ana makosa hata awe anafanya ibada vipi, kwa hiyo ni neema kwetu kuzidishiwa fadhila kwa kutekeleza vitendo vya Sunnah fulani ili kujiongezea thawabu na daraja ya Pepo kwani hakuna mtu asiyependa ziada ya neema.
Fadhila ya Kuswaliwa na Allaah سبحانه وتعالى mara kumi
عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص ، رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ : (( من صلَّى عليَّ صلاَةً ، صلَّى اللَّه علَيّهِ بِهَا عشْراً)) رواهُ مسلم
Imetoka kwa 'Abdullah ibn 'Amru ibn Al'Aasw رضي اللَّه عنْهُمَا kwamba kamsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم anasema, ((Atakayeniswalia Swalah moja Allaah Atamswalia mara kumi)) [Muslim]
Maana ya Swalah ya Allaah سبحانه وتعالى na Malaika Wake:
Swalah ya Allaah سبحانه وتعالى kwa waja Wake ni: Rahma na kuwasifu kwa malaika.
Swalah ya Malaika kwa waumini ni:
Du'aa na kuwaombea maghfirah.
Kupata daraja ya Pepo karibu naye Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :
عن ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : (( أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم عَليَّ صلاةً)) رواه الترمذي وقال : حديثٌ حسنٌ
Imetoka kwa ibn Mas'uud رضي اللَّه عنْهُ kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
amesema, ( (watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu) siku
ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia
[At-Tirmidhy na kasema ni Hadiythi Hasan]
Vile vile kumuombea Du'aa, mfano du'aa baada ya adhaan ni fadhila kwetu kuwa atakayefanya hivyo atakuwa miongoni mwa atakayeombewa Shufaa na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
4) Kudhihirisha mapenzi yetu kwake
Muumini ni yule mwenye kumpenda khaswa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kabla ya kupenda chochote hata nafsi yake kwani ilipoteremka aya hii:
((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ))
((Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao)) [Al-Ahzaab:6].
'Umar رضي الله عنه alisema kuwa yeye anampenda Mtume kuliko chochote ila nafsi yake. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia 'Umar kuwa hadi ampende hata kuliko nafsi yake ndipo yatakapothibitika mapenzi yake, naye 'Umar akakubali kuwa anampenda kuliko hata nafsi yake. Kwa hiyo na sisi waumini tuwe na mapenzi makubwa ya kumpenda na dalili mojawapo ni kupenda kumswalia.
5) Kumswalia kwetu ni thawabu alizokwishaahidiwa.
Allaah سبحانه وتعالى Amekwishamuahidi Mtume Wake kuwa atapata malipo mengi yasiyokatika:
((وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ))
((Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika)) [Al-Qalam: 3]
Mbali ya kuwa ni malipo yake kwa sababu ya utume wake na kufikisha ujumbe kwa tabu na maudhi, vile vile kumswalia kwetu kila siku
Mwisho kama ulivyosema kuwa sisi ndio tuliokuwa njia panda na tunaohitaji kuombeana, bila shaka tunahitaji kufanya hivyo, na kwa hiyo pia kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kutuzidishia uzito wa mizani zetu za mambo mema na kufanya nyepesi mizani za mambo maovu.
Wa Allaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
