16-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Hakumwita Kwa Jina Lake Katika Qur-aan Kama Walivoitwa Manabii Wengineo

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

16-Allaah Hakumwita Kwa Jina Lake Katika Qur-aan Kama Walivoitwa Manabii Wengineo

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Kwa sababu ya utukufuu wake na heshima kubwa Aliyopewa, ni Nabiy pekee ambaye Allaah ('Azza wa Jalla) Hakumwita kwa jina lake bali Alimwita  kwa cheo chake cha Rasuli au Nabiy; mifano michache ifuatayo:  

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ  

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako.  [Al-Maaidah: 67]

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji. [Al-Ahzaab: 45]

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ  

Ee Nabiy!  Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda.  [Atw-Twalaaq: 1]

 

 

Na hata katika hali nyengine Allaah ('Azza wa Jalla) Alimwita kwa sifa fulani badala ya jina lake, mfano:

 

 

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾

Ee uliyejifunika. [Al-Muzzammil: 1]

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

Ee mwenye kujigubika! [Al-Muddath-thir: 1]

 

 

Lakini jina lake Amelitaja Allaah ('Azza wa Jalla) katika hali ya kujulishwa kuhusu khabari zake ndipo Amemtaja kwa jina lake, mfano watu kujulishwa kuwa yeye ni Rasuli wa Allaah, wala sio kumwita kwa "Yaa Muhammad".

 

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ  

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao [Al-Fat-h]

 

Na pia,

 

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ  

Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) si yeyote isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rusuli.  [Aal-‘Imraan: 144]

 

 

Na pia:

 

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.  [Al-Ahzaab: 40]

 

 

 

Mifano ya Manabii walioitwa kwa majina yao katika hali ya kuitwa na kutajwa khabari zao:

 

 

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

Na Tukasema: Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu. [Al-Baqarah: 35]

 

 

 قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ

Pakasemwa: “Ee Nuwh!  Teremka (jahazini) kwa amani kutoka Kwetu na Baraka nyingi juu yako, na juu za umati zilio pamoja na wewe. [Huwd: 48]

 

 

وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾

Tukamwita: “Ee Ibraahiym. [Asw-Swaffaat: 104]

 

 

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

 

. (Akaambiwa): “Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.” [Maryam: 7]

 

 

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾

(Alipofikia kimo cha kufahamu aliambiwa) “Ee Yahyaa!  Chukua Kitabu kwa nguvu.” Na Tukampa Al-Hukma (hikma, ufahamu wa shariy’ah, elimu n.k) angali mtoto. [Maryam: 12]

 

 

Katika hali ya kumwita Muwsaa (‘Alayhis-salaam):

 

 

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

 

(Allaah) Akasema: “Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekuteua juu ya watu kwa ujumbe Wangu na maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”  [Al-A’raaf: 144]

 

 

Katika hali ya kujulisha khabari zake. Mfano wachawi walipomwambia Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam):

 

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾

(Wachawi) Wakasema: Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa (kwanza) kutupa.   [Al-A’raaf: 115]

 

 

Mfano wa katika hali ya kumwita Nabiy ‘Iysaa (‘Alayhis-salaam):

 

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!  Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) Atasema: Utakasifu ni Wako hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu; na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako; hakika Wewe ni Mjuzi wa ghayb. [Al-Maaida: 116]

 

Na katika hali ya kujulisha khabari zake:

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu, Tuteremshie meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku. [Al-Maaidah: 114]

 

 

Share