Kuandama Mwezi – Afuate Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?
SWALI:
Assalaamu alaikum,
Je nifunge lini,pale mwezi unapoandama sehemu
yoyote ya dunia au mpaka utangazwe na viongozi wa kidini katika Nchi yangu.
Kwa leo ni hayo tuu.
Ndugu yenu katika uislam
JIBU
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Kauli iliyo sahihi na yenye nguvu ni kufunga kwa kuonekana popote mwezi. Hadiyth mbalimbali zimeonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifunga kwa taarifa za mwezi kutoka sehemu mbalimbali na vile alifungua kutokana na taarifa zilizomjia bila hata yeye kuuona mwezi. Suala hili ni refu na dalili ni nyingi.
Uislam hauna mipaka, na popote duniani Muislam atakapouona mwezi, basi anapaswa Muislam aliyesikia taarifa hizo kufunga bila kujali yuko nchi gani au mji gani. Yasemwayo kuhusu kufunga kwa kiwango cha masafa au kipimo cha vitongoji au ukaribu wa majimbo, miji na nchi, hili halina dalili katika sheria bali ni jitihada za wanachuoni.
Na mojawapo ya fadhila za kutekeleza matendo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kufunga kwa kuonekana mwezi popote, ni kupatikana kwa umoja na mshikamano baina ya Waislam kila sehemu duniani. Na ndipo panapoweza vilevile kupatikana siku moja ya 'Iyd duniani na Waislam wote wakawa katika furaha na sherehe pamoja.
Khitilafu na fitna tunazoziona leo hii za kufunga tofauti na kula 'Iyd tofauti hadi kufikia wengine wakila 'Iyd mwanzo hupigwa na kudhibitiwa na dola, ni matunda ya kutofahamika na kutofuatwa matendo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na pia baadhi ya Waislam kushikamana na masimulizi ya Kurayb yenye utata na kuacha matendo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yasiyo na shaka wala khitilafu.
Kwa maelezo zaidi soma mada katika kiungo kifuatacho:
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Namshukuru Allah kwa
Namshukuru Allah kwa kunijaalia kutoa maoni yangu kuhusu mwandamo wa mwezi. Ni kweli kabisa ipo hadithi kuwa mtume(SAW) aliwahi kufunga na kufungua kwa taarifa za kuambiwa bila ya yeye mwenyewe kuuona mwezi. Pia ipo hadithi kuwa Mtume aliwahi kuwatembelea waislamu wa nchi jirani siku ya Iydd akawakuta bado wamefunga,akawauliza kuwa hawajapata taarifa ya kuonekana mwezi? wakasema laa!! basi akawambia wakamilishe siku, wakafanya hivyo na hakuna yeyote aliyesema kuwa wamefunga siku ya iydd kama tunavyoamini kuwa ni haramu kufunga siku ya iydd. Hivyo napenda kuwaambia ndugu zangu waislamu tena hususani watanzania kuwa, kufunga ni kuonekana mwezi popote duniani endapo tu utapewa taarifa na mtu ambaye ni mwislamu wa kuaminika au atakeyekuabali kushahadia ili kuthibitisha taarifa hiyo ni ya kweli kama alivyofanya Mtume(SAW) kutokana na taarifa aliyopewa na mtu mmoja kutoka mashambani. Allah ndio mjuzi zaidi.
Mwisho wa yote nawatakia waislamu wooote Tanzania na Duniani kwa ujumla ramadhani njema na yenye athari ndani ya nyoyo zetu kutu INSA'ALLAH.
Assalaamu
Assalaamu 'alaykum
Tunakushukuru kwa maoni yako mazuri, na tumefurahi kuona kwamba mafunzo ya dini Swahiyh tunayowakusanyia yanaleta faida kwenu.
Tunazidi kumuomba Allaah Subhaanah wa Ta'ala Aturuzuku ikhlaasw, Atufanyie wepesi na Atutakabalie nanyi msitusahau kwa du'aa.