Hilaal: Mwandamo Wa Mwezi Upi Sahihi Wa Kitaifa Au Kimataifa?

 Mwandamo Wa Mwezi Upi Sahihi Wa Kitaifa Au Kimataifa?

 

www.alhidaay.com

 

 

SWALI:

 

 Ni upi mwandamo sahihi wa mwezi kati ya mwezi wa kimataifa na kitaifa. 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Suala la mwandamo wa mwezi, ni suala lenye ikhtilaaf baina ya ‘Ulamaa.

 

Lakini mtazamo sahihi kwa nguvu za dalili zake, ni mwandamo wa popote pale unapoandama, Muislamu anapaswa kufunga na kufungua.

 

Hata hivyo, mas-alah haya kama tulivyotangulia kusema, ni yenye ikhtilaaf. Hakuna haja ya Waislamu kuzozana wala kugombana wala upande mmoja kukemea upande wa wengine.

 

Hapa chini kwenye kiungo utapata majibu mbalimbali ya kupanua ufahamu katika suala hilo:

 

Mwandamo Wa Mwezi; Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?

 

Kufuata Mwezi Wa Kitaifa Au Wa Kimataifa; Kupishana Masaa; Wazee Zamani Walikuwa Wanapataje Habari Kuhusu Mwezi Wa Kimataifa

 

Mwandamo Wa Mwezi – Waislamu Wote Duniani Wafunge Siku Moja Na Kula ‘Iyd Siku Moja ?

 

Utata wa Kufunga Swawm na Kufungua Kutokana Na Kutofautiana Kuhusu Mwandamo Wa Mwezi

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share