097 - Al-Qadr
الْقَدْر
Al-Qadr: 097
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul-Qadr (Usiku wa Qadr).
وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾
2. Na nini kitakachokujulisha ni nini Laylatul-Qadr?
لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾
3. Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.
تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾
4. Wanateremka humo Malaika pamoja na Ar-Ruwh (Jibriyl) kwa Idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.
سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾
5. Usiku huo ni amani mpaka kuchomoza Alfajiri.
