Skip to main content
⌂
Alhidaaya.com homepage
slogan image
  • Log in

left sidebar menu

  • Qur-aan
  • Hadiyth
  • Sunnah
  • Tawhiyd
  • Aqiydah
  • Manhaj
  • Shirki & Kufru
  • Bid-'ah (Uzushi)
  • Salaf Wa Ummah
  • Firaq-Makundi
  • Fiqh-Ibaadah
  • Duaa-Adhkaar
  • Fataawa Za Ulamaa
  • Kauli Za Salaf
  • Akhlaaq-Aadaab
  • Raqaaiq
  • Familia-Jamii
  • Maswali-Majibu
  • Chemsha Bongo
  • Vitabu
  • Mapishi

022-Unawezaje Kuupata Moyo Wa Mumeo Na Kumridhisha Mola Wako: Kwenye Njia Panda

KWENYE NJIA PANDA

Ewe, mke Muumini, kila mtu husogea katika furaha lakini wachache ndio wanaopata, wengi wao hukosea njia yake. Ama sisi Waislamu tunajua ya kwamba furaha ya kweli huanzia mwanzo kabisa kwa imani ya mtu kwa Mola wake na utiifu wake na kufuata mfumo na shari’ah Zake.

Ukitaka ewe Dada yangu Muumini kupata furaha ya kweli kabisa ni juu yako kubadilisha muelekeo, nayo si mwengine bali utiifu kwa mume wako, huwa ndio chanzo cha utiifu wako kwa Mola wako na kumridhisha mume wako ndio kumridhisha Mola wako na haya ndio ambayo yatakufanya umsamehe makosa yake na kuangalia thawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kabla ya kutaka ujira wa hapa hapa duniani au kuridhia kwa mume wako na kuukabili ubaya uliofanyiwa kwa wema utakaoufanya na yote ni kufuata maelekezo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) aliposema,

“…Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa aliye mpole.” (41: 34)

Hii kwa Yule ambaye ana ugomvi na mwenzake, lakini je kwa yule ambaye ana usuhuba na mwenzake, mapenzi na huruma itakuwaje?!!

Wema ni wema ewe dada yangu, hifadhi maneno haya saba yafuatayo yatakufaa na ndio mwisho wa risala yangu hii.

1.     Utiifu (kwa Mola wako kisha kwa mume wako kwa sharti utiifu huo kwa mume wako usiwe ni katika kumuasi mola wako);

2.     Kukinai;

3.     Kuwa mwaminifu;

4.     Fanya mambo yako bila ya kujikalifisha, yaani fanya mambo yako kwa wepesi;

5.     Kuwa msafi daima;

6.     Kuwa ni mwenye tabasamu muda wote;

7.     Daima mpendelee mwenzako.

Mwisho Wa Risala Hii


Book traversal links for Unawezaje Kuupata Moyo Wa Mumeo Na Kumridhisha Mola Wako

  • ‹ 021-Unawezaje Kuupata Moyo Wa Mumeo Na Kumridhisha Mola Wako: Jirani Ana Haki Tusizisahau
  • Up
moon-icon

Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

  • Muharram
    image
    مُحَرَّمْ
  • Swafar
    image
    صَفَرْ
  • Rabiy’u Al-Awwal
    Rabiy’u Al-Awwal
    رَبيعُ الْأَوًّلْ
  • Rabiy'u Al-Aakhir
    Rabiy'u Al-Aakhir
    رَبيعُ الآخِرْ
  • Jumaadaa Al-Uwlaa
    image
    جُمَادَى الْأُوْلَى
  • Jumaadaa Al-Aakhirah
    image
    جُمَادَى الْآخِرَة
  • Rajab
    image
    رَجَبْ
  • Sha'baan
    Shabaan
    شَعْبَانْ
  • Ramadhwaan
    iocn
    رَمَضَانْ
  • Shawwaal
    image
    شَوّالْ
  • Dhul-Qa’dah
    image
    ذُو الْقَعْدَةْ
  • Dhul-Hijjah
    icon
    ذُو الحِجَّةْ
Alhidaaya.com homepage
  • Kuhusu Alhidaaya
  • Maoni Yako-Wasiliana Na sisi (Contact Us)
  • Tovuti Muhimu

© 2026 Alhidaaya.com All rights reserved.