Skip to main content

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)063-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Istisqaa (Kuomba Mvua)

Hiswnul-Muslim

063-Du’aa Ya Istisqaa (Kuomba Mvua)

www.alhidaaya.com

Bonyeza Hapa Usikilize

[169] 

اللّهُمَّ اَسْقِـنا غَيْـثاً مُغيـثاً، مَريئاً، مُريـعاً، نافِعـاً غَيْـرَ ضَّارٌ، عاجِـلاً غَـيْرَ آجِلٍ

Allaahumma Asqinaa ghaythan mughiythaa, mariy-aa, muriy’aa, naafi’an ghayra dhwaarun, ’aajilan ghayra aajil

Ee Allaah Tunyesheleze mvua yenye kuokoa, nyingi yenye kustawisha, yenye manufaa isiyo dhuru, ya haraka isiyochelewa[1]

[170]

اللّهُمَّ أغِثْنـَا، اللّهُمَّ أغِثْنـَا، اللّهُمَّ أغِثْنـَا

Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa

Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa kututeremshia mvua, Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa kututeremshia mvua, Ee Allaah tunakuomba utuokowe kwa kututeremshia mvua[2]

[171]

اللّهُمَّ اسْقِ عِبادَكَ وَبَهـائِمَك، وَانْشُـرْ رَحْمَـتَكَ وَأَحْيِي بَلَـدَكَ المَيِّـت

Allaahummasqi ’ibaadaka, wa bahaaimaka, wanshur Rahmataka wa Ahyi baladakal-mayyit

Ee Allaah Wanyesheleze waja Wako, na wanyama Wako, na Eneza Rehma Zako na Fufua nchi Yako iliyokufa[3]

 

[1]Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdullaah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (1/303) [1169], ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/216).

[2]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (1/224)[ 1013], Muslim (2/613) [897].

[3]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amruw bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما)  - Abu Dawwud (1/305) [1176], na Al-Albaaniy (رحمه الله) ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/218)