Kauli Za Salaf: Jamii
Suhubianeni Na Swaalihina (Waja Wema) Ili Muwe Nao Au Muwe Kama Wao
Imaam Qataadah (Rahimahu Allaah)
Imaam Qataadah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakika sisi, Wa-Allaahi, hatukupata kuona mtu anayesuhubiana na watu isipokuwa huwa mfano wake na shakili yake. Basi suhubianeni na Swaalihina enyi waja wa Allaah, ili muwe pamoja nao na huenda mkawa mfano wao.”
[Al-Ibaanah (2/477)]