Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

025-Suwrah Al-Furqaan Aayah 27 - 29

 

 

Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾ يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾ لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾

Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli.  Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani. Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia. Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza. [Al-Furqaan (25): 27, 28, 29]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عن ابن عباس رضي الله عنهما أن أبا مُعَيط - وهو عقبة بن أبي معيط - كان يَجلِسُ مع النبي صلى الله عليه وسلم بمكةَ لا يُؤذيه، وكان رجلاً حليمًا، وكان بقيَّةُ قريشٍ إذا جَلَسوا آذَوْه، وكان لأبي مُعيطٍ خليلٌ غائبٌ عنه بالشام (هو أبي بن خلف الجمحي) فقالت قريشٌ: صَبَأَ أبو مُعَيط. وقدِم خليلُه من الشام ليلاً، فقال لامرأته: ما فَعَل محمدٌ مما كان عليه؟ فقالت: أشدُّ مما كان أمرًا. فقال: ما فَعَل خليلي أبو مُعَيط؟ فقالت: صبَأ. فبات بليلةِ سَوءٍ، فلما أصبَح أتاه أبو مُعَيط فحَيَّاه، فلم يرُدَّ عليه التحيةَ، فقال: ما لكَ لا تَرُدُّ عليَّ تحيتي؟ فقال: كيف أَرُدُّ عليك تحيَّتَك وقد صَبَوتَ؟ قال: أَوَ قَدْ فَعَلَتْها قريش؟ قال: نعم. قال: فما يُبرئُ صُدورَهم إِنْ أنا فعلتُ؟ قال: تأتيه في مَجلِسِه فتبزُقُ في وجهه، وتشتُمُه بأخبثِ ما تعلمُ من الشَّتْم. ففعل، فلم يَزد النبيُّ صلى الله عليه وسلم على أن مَسَح وجهه من البُزاق، ثم التفت إليه فقال: "إِنْ وَجَدْتُكَ خَارِجًا مِنْ جِبَالِ مَكَّةَ أَضْرِبُ عُنُقَكَ صَبْرًا" فلمَّا كان يومُ بدرٍ وخَرَج أصحابُه، أبى أن يخرجَ، فقال له أصحابه: اخرجْ معنا. قال: قد وَعَدَني هذا الرجل إن وَجَدَني خارجًا من جبال مكةَ أن يضربَ عُنُقي صبرًا. فقالوا: لك جَمَلٌ أحمرُ لا يُدْرَك، فلو كانتِ الهزيمةُ طِرْتَ عليه، فخرج معهم، فلما هَزَم اللهُ المشركين، وَحَلَ  به جَمَلُه في جَدَدٍ  من الأرض، فأخذه رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أسيرًا في سبعينَ مِن قُرَيْش، وقدِم إليه أبو مُعَيط، فقال: أتقتلُني مِن بين هؤلاء؟ قال: "نَعَمْ، بِمَا بَزَقْتَ فِي وَجْهِي". فأنزل الله في أبي مُعَيْط: ((وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَى يَدَيْهِ)) إلى قوله: ((وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلإِنسَانِ خَذولاً ))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kuwa Abu Mu’aytw alikuwa akikaa majilisi pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) mjini Makkah bila kumfanyia maudhi wala vitimbi vyovyote. Alikuwa mtu mkarimu, mpole na mwenye kujiheshimu. Lakini Maquraysh wengine walikuwa wakimuudhi na kumtaabisha sana Rasuli wanapokaa pamoja naye. Abu Mu’aytw alikuwa na rafiki yake mwandani (Ubayya bin Khalaf Al-Jumahiy) ambaye alikuwa amesafiri kwenda Sham. (Na kutokana na kukaa kwake vyema pamoja na Rasuli bila kumfanyia bughudha) Maquraysh walisema: Abu Mu’aytw ameiacha Dini yake (na kufuata dini ya Muhammad). Rafiki yake mwandani (Ubayya bin Khalaf Al-Jumahiy) akarudi toka Sham usiku, na akamuuliza mkewe kuhusu nini kafanya Muhammad kukabiliana na mizengwe na vitimbi anavyofanyiwa. Akamjibu kuwa mambo yamezidi kuliko yalivyokuwa. Akamuuliza: Na vipi rafiki yangu kipenzi Abu Mu’aytw? Akamwambia: Ameacha Dini yake.  Akalala  usiku mbaya kabisa. Kulipopambazuka, Abu Mu’aytw alimwendea, akamsalimia lakini hakumjibu salaam yake. Akamuuliza: Kunani? Mbona hunijibu salaam yangu? Akamwambia: Vipi nitakujibu salaam yako na wewe ushaacha dini yako? Akamuuliza: Je, Maquraysh pia wameamua hivi? Nifanye jambo gani ili waniridhie? Akamwambia: Nenda kwenye majilisi yake, umtemee mate usoni, kisha mtukane matusi yote machafu ya nguoni unayoyajua. Akaenda na kutekeleza hilo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) hakujibisha lolote zaidi ya kuyafuta mate usoni mwake, akamgeukia na kumwambia: Nikikupata nje ya milima ya Makkah, basi nitakukata shingo baada ya kukuteka na kukufunga kwenye kigogo. Na siku ya (vita vya) Badr ilipowadia, na wenzake wakajitayarisha kutoka, yeye alikataa kutoka nao. Masahibu zake wakamsihi atoke, lakini aliwaambia: Huyu mtu ameniahidi (ahadi ya onyo) kuwa akinikuta nje ya milima ya Makkah, basi atanifyeka shingo baada ya kuniteka na kunifunga. Wakamwambia kuwa watampa ngamia mwekundu ambaye hakamatiki kwa mbio, na kama watashindwa, basi ngamia ataruka naye juu kutokana na kasi yake, hivyo akaamua kutoka nao. Na Allaah Alipowashinda washirikina, na ngamia wake akatuama naye kwenye ardhi tambarare, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alimchukua kama mateka na kumjumuisha na mateka wengineo sabiini wa Kiquraysh. Abu Mu’aytw akamwendea na kumuuliza: Je, utaniua mimi tu kati ya hawa? Akamwambia: “Na’am, kwa sababu ya kunitemea mate usoni.” Hapo Allaah ‘Azza wa Jalla Akateremsha kumzungumzia Abu Mu’aytw:

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

024-Suwrah An-Nuwr Aayah 61

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَامِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَالِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَالَاتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَأْكُلُوا جَمِيعًا أَوْ أَشْتَاتًا ۚ فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٦١﴾

Si vibaya kwa kipofu, na wala si vibaya kwa kilema, na wala si vibaya kwa mgonjwa, na wala nyinyi wenyewe kama mtakula majumbani mwenu, au majumbani mwa baba zenu, au majumbani mwa mama zenu, au majumbani mwa kaka zenu, au majumbani mwa dada zenu, au majumbani mwa ‘ammi zenu, au majumbani mwa shangazi zenu, au majumbani mwa wajomba zenu, au majumbani mwa makhalati zenu au za mliowashikia funguo zao, au rafiki yenu. Hakuna ubaya kama mkila pamoja au mbali mbali. Mtakapoingia majumbani toleaneni salaam; maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. Hivyo ndivyo Anavyokubainishieni Allaah Aayaat ili mpate kutia akilini. [An-Nuwr:  61]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

024-Suwrah An-Nuwr Aayah 55

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٥٥﴾

Allaah Amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba bila shaka Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao, na bila shaka Atawamakinishia Dini yao Aliyowaridhia, na bila shaka Atawabadilishia amani badala ya khofu yao; wawe wananiabudu Mimi wasinishirikishe na chochote; na yeyote yule atakayekufuru baada ya hapo, basi hao ndio mafasiki. [An Nuwr (24:56)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

024-Suwrah An-Nuwr Aayah 33

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَالَّذِينَ يَبْتَغُونَ الْكِتَابَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖوَآتُوهُم مِّن مَّالِ اللَّـهِ الَّذِي آتَاكُمْ ۚ وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wajisitiri (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe katika fadhila Zake. Na wale wanaotaka kuandikiwa kuachiwa huru katika wale ambao imemiliki mikono yenu ya kuume, basi waandikieni kama mkijua wema kwao. Na wapeni katika mali ya Allaah Aliyokupeni. Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko, ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.     [An Nuwr (24:33)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، وَأَبُو كُرَيْبٍ جَمِيعًا عَنْ أَبِي مُعَاوِيَةَ، - وَاللَّفْظُ لأَبِي كُرَيْبٍ - حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ كَانَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ يَقُولُ لِجَارِيَةٍ لَهُ اذْهَبِي فَابْغِينَا شَيْئًا فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ:  ‏((‏وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Ametuhadithia Abu Bakr bin Abiy Shaybah na Abu Kurayb, na wote wawili toka kwa Mu’aawiyah – na tamshi ni la Abu Kurayb – ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, ametuhadithia Al-A’amash toka kwa Abu Sufyaan toka kwa Jaabir amesema: ‘Abdullaah bin Ubayya bin Saluwl alikuwa akimwambia kijakazi wake: Toka nenda ukajitembeze utuletee chochote. Na hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:

 

وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ  فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko [hao vijakazi], ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

[Muslim katika Mujallad wa 18 ukurasa wa 162]

 

Pia, ...

 

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Suwrah An-Nuwr Aayah 11 - 22

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١﴾

Hakika wale walioleta singizo la kashfa; (kumzulia mama wa waumini ‘Aaishah  رضي الله عنها) ni kundi miongoni mwenu. Msiichukulie kuwa ni shari kwenu, bali ni khayr kwenu.  Kila mtu katika wao atapata yale aliyochuma katika dhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kuu.

[An-Nuwr Kuanzia Aayah ya 11 hadi ya 22]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Asbaabun-Nuzuwl

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

048-Al-Fat-h Aayah 24 - 26

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُم بِبَطْنِ مَكَّةَ مِن بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا﴿٢٤﴾ هُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْيَ مَعْكُوفًا أَن يَبْلُغَ مَحِلَّهُ ۚوَلَوْلَا رِجَالٌ مُّؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُّؤْمِنَاتٌ لَّمْ تَعْلَمُوهُمْ أَن تَطَئُوهُمْ فَتُصِيبَكُم مِّنْهُم مَّعَرَّةٌ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ لِّيُدْخِلَ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ لَوْ تَزَيَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٢٥﴾ إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ التَّقْوَىٰ وَكَانُوا أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا﴿٢٦﴾

Naye Ndiye Aliyeizuia mikono yao dhidi yenu na mikono yenu dhidi yao katikati ya Makkah baada ya kukupeni ushindi juu yao. Na Allaah daima ni Mwenye kuona yale myatendayo. Wao ndio wale waliokufuru na wakakuzuieni na Al-Masjidil-Haraam na wanyama wa kuchinjwa wakazuiliwa kufika mahali pa kuchinjwa. Na ingekuwa si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua nyinyi, mkawasaga kuwaua na kwa sababu yao yakakusibuni madhambi (na fedheha) bila ya kujua, ili Allaah Amuingize katika rahmah Yake Amtakaye…na lau kama (Waumini na makafiri) wangelitengana; bila shaka Tungeliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo. Walipotia katika nyoyo zao ghadhabu na kiburi; ghadhabu na kiburi za kipindi cha ujahili Allaah Akateremsha utulivu Wake juu ya Rasuli Wake na juu ya Waumini na Akawalazimisha neno la Taqwa (laa ilaaha illa-Allaah), na wakawa ndio wenye haki zaidi kwalo na wenye kustahiki. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu.

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

24-Suwrah An-Nuwr Aayah 6 - 9

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٧﴾وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٨﴾وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّـهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٩﴾

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli. Na (kiapo) cha tano kwamba laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo. Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo. Na (kiapo) cha tano kwamba ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. [An-Nuwr: 6 – 9]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي عَدِيٍّ، عَنْ هِشَامِ بْنِ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا عِكْرِمَةُ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ هِلاَلَ بْنَ أُمَيَّةَ، قَذَفَ امْرَأَتَهُ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِشَرِيكِ بْنِ سَحْمَاءَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ الْبَيِّنَةَ أَوْ حَدٌّ فِي ظَهْرِكَ ‏"‏‏.‏ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِذَا رَأَى أَحَدُنَا عَلَى امْرَأَتِهِ رَجُلاً يَنْطَلِقُ يَلْتَمِسُ الْبَيِّنَةَ‏.‏ فَجَعَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ الْبَيِّنَةَ وَإِلاَّ حَدٌّ فِي ظَهْرِكَ ‏"‏ فَقَالَ هِلاَلٌ وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ إِنِّي لَصَادِقٌ، فَلَيُنْزِلَنَّ اللَّهُ مَا يُبَرِّئُ ظَهْرِي مِنَ الْحَدِّ، فَنَزَلَ جِبْرِيلُ، وَأَنْزَلَ عَلَيْهِ ‏ وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ‏  فَقَرَأَ حَتَّى بَلَغَ ‏ ‏إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ‏ فَانْصَرَفَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَرْسَلَ إِلَيْهَا فَجَاءَ هِلاَلٌ، فَشَهِدَ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ أَنَّ أَحَدَكُمَا كَاذِبٌ فَهَلْ مِنْكُمَا تَائِبٌ ‏"‏‏.‏ ثُمَّ قَامَتْ فَشَهِدَتْ فَلَمَّا كَانَتْ عِنْدَ الْخَامِسَةِ وَقَّفُوهَا، وَقَالُوا إِنَّهَا مُوجِبَةٌ‏.‏ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فَتَلَكَّأَتْ وَنَكَصَتْ حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّهَا تَرْجِعُ ثُمَّ قَالَتْ لاَ أَفْضَحُ قَوْمِي سَائِرَ الْيَوْمِ، فَمَضَتْ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَبْصِرُوهَا فَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أَكْحَلَ الْعَيْنَيْنِ سَابِغَ الأَلْيَتَيْنِ خَدَلَّجَ السَّاقَيْنِ، فَهْوَ لِشَرِيكِ بْنِ سَحْمَاءَ ‏"‏‏.‏ فَجَاءَتْ بِهِ كَذَلِكَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَوْلاَ مَا مَضَى مِنْ كِتَابِ اللَّهِ لَكَانَ لِي وَلَهَا شَأْنٌ ‏"‏‏

 

Amenihadithia Muhammad bin Bashshaar, ametuhadithia Ibn Abiy ‘Adiyy kutoka kwa Hishaam bin Hassaan, ametuhadithia ‘Ikrimah, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa Hilaal bin Umayyah  alimshutumu mkewe (kuwa amezini) na Shariyk bin Sahmaa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia (Hilaal): “Lete ubainifu (mashahidi wanne) au hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy’ah ya viboko) mgongoni mwako”. Hilaal akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mmoja wetu anapomuona mwanamme juu ya mkewe atoke kwenda kutafuta mashahidi? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kumwambia, “Ima ulete ubainifu (wa mashahidi wanne) au hadd mgongoni mwako”. Hapo, Hilaal  akasema: “Naapa kwa Yule Aliyekutuma kwa haki, hakika mimi ni mkweli na Allaah Atateremsha kitakacho usalimisha mgongo wangu na hadd”. Jibriyl akateremka na kumteremshia: ...

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

24- Suwrah An-Nuwr Aayah 3

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini. [An Nuwr (24:3)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ الأَخْنَسِ، أَخْبَرَنِي عَمْرُو بْنُ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ كَانَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ مَرْثَدُ بْنُ أَبِي مَرْثَدٍ وَكَانَ رَجُلاً يَحْمِلُ الأَسْرَى مِنْ مَكَّةَ حَتَّى يَأْتِيَ بِهِمُ الْمَدِينَةَ قَالَ وَكَانَتِ امْرَأَةٌ بَغِيٌّ بِمَكَّةَ يُقَالُ لَهَا عَنَاقُ وَكَانَتْ صَدِيقَةً لَهُ وَإِنَّهُ كَانَ وَعَدَ رَجُلاً مِنْ أُسَارَى مَكَّةَ يَحْمِلُهُ قَالَ فَجِئْتُ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى ظِلِّ حَائِطٍ مِنْ حَوَائِطِ مَكَّةَ فِي لَيْلَةٍ مُقْمِرَةٍ ‏.‏ قَالَ فَجَاءَتْ عَنَاقُ فَأَبْصَرَتْ سَوَادَ ظِلِّي بِجَنْبِ الْحَائِطِ فَلَمَّا انْتَهَتْ إِلَىَّ عَرَفَتْهُ فَقَالَتْ مَرْثَدُ فَقُلْتُ مَرْثَدُ ‏.‏ فَقَالَتْ مَرْحَبًا وَأَهْلاً هَلُمَّ فَبِتْ عِنْدَنَا اللَّيْلَةَ ‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا عَنَاقُ حَرَّمَ اللَّهُ الزِّنَا ‏.‏ قَالَتْ يَا أَهْلَ الْخِيَامِ هَذَا الرَّجُلُ يَحْمِلُ أَسْرَاكُمْ ‏.‏ قَالَ فَتَبِعَنِي ثَمَانِيَةٌ وَسَلَكْتُ الْخَنْدَمَةَ فَانْتَهَيْتُ إِلَى كَهْفٍ أَوْ غَارٍ فَدَخَلْتُ فَجَاءُوا حَتَّى قَامُوا عَلَى رَأْسِي فَبَالُوا فَطَلَّ بَوْلُهُمْ عَلَى رَأْسِي وَأَعْمَاهُمُ اللَّهُ عَنِّي ‏.‏ قَالَ ثُمَّ رَجَعُوا وَرَجَعْتُ إِلَى صَاحِبِي فَحَمَلْتُهُ وَكَانَ رَجُلاً ثَقِيلاً حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى الإِذْخِرِ فَفَكَكْتُ عَنْهُ كَبْلَهُ فَجَعَلْتُ أَحْمِلُهُ وَيُعِينُنِي حَتَّى قَدِمْتُ الْمَدِينَةَ فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنْكِحُ عَنَاقًا مَرَّتَيْنِ فَأَمْسَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلَمْ يَرُدَّ عَلَىَّ شَيْئًا حَتَّى نَزَلَتِ ‏:‏ ((الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ‏))  فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَا مَرْثَدُ الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ فَلاَ تَنْكِحْهَا ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ ‏.‏

 

Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Rawh bin ‘Ubaadah toka kwa ‘Ubaydullaa bin Al-Akhnas amesema: Amenieleza ‘Amri bin Shu’ayb akipokea toka kwa baba yake toka kwa babu yake aliyesema: Kulikuwa na mtu ajulikanaye kama Marthad. Kazi yake ilikuwa ni kuwabeba na kuwatorosha mateka toka Makkah kuwaleta Madiynah. Na hapo Makkah alikuwepo mwanamke kahaba aitwaye ‘Anaaq ambaye alikuwa ni hawara yake Marthad (kabla hajasilimu). Marthad alikuwa amemwahidi mtu mmoja katika mateka wa Makkah kuwa atambeba (kumtorosha). [Marthad anasema]: Nikaja hadi nikaishilia katika kivuli cha kuta kati ya kuta za Makkah katika usiku angavu wa nuru ya mwezi. ‘Anaaq akaja, akaona weusi wa kivuli changu pembeni ya ukuta. Aliponifikia, alinitambua akasema: Ni Marthad! Nami nikasema ni (mimi) Marthad. Akasema: Karibu sana, njoo basi ulale kwetu usiku huu. Nikamwambia: Ee ‘Anaaq! Allaah Ameharamisha zinaa! (Hapo hapo) akapiga ukelele na kusema: Enyi watu wa makhema! Huyu hapa mtu anayewatorosha mateka wenu. Watu wanane wakaniandama, nikapita Al-Khandamah, nikakimbilia pangoni na kuingia. Wakaja mpaka wakasimama juu ya kichwa changu (mdomo wa pango) lakini Allaah Aliwaziba macho wasiweze kuniona. Kisha wakaondoka, nami nikarudi kwa mwenzangu, nikambeba, naye alikuwa mzito. Nikamfuata mwingine, nikamfungua minyonyoro yake, nikaanza kumbeba huku akinilemea na kunichosha mpaka nikawasili Madiynah. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Je, naweza kumwoa ‘Anaaq? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akanyamaza, hakujibu kitu mpaka iliposhuka:

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 023-Asbaabun-Nuzuwl Al-Muuminuwn Aayah 76

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Kwa yakini Tuliwachukua kwa adhabu, basi hawakunyenyekea kujisalimisha kwa Rabb wao, na wala hawakuomba du’aa kwa raghba na khofu. [Al-Muuminuwn: 76]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حدثنا ابن حميد قال حدثنا أبو تميلة هو يحيى بن واضح عن الحسين عن يزيد عن عكرمة عن ابن عباس قال: جاء أبو سُفيانَ بنُ حَرْبٍ إلى رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقال : يا مُحمَّدُ أنشُدُكَ اللهَ والرَّحِمَ فقد أكَلْنا العِلْهِزَ - يعني الوَبَرَ والدَّمَ - فأنزَل اللهُ  وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Ametuhadithia Ibn Humayd amesema: Ametuhadithia Abu Thamiylah ambaye ni Yahyaa bin Waadhwih, toka kwa Al-Husayn, toka kwa ‘Ikrimah, toka kwa Ibn ‘Abbaas, amesema: Abu Sufyaan (bin Harb, kiongozi wa Maquraysh]) alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Muhammad!  Nakuomba uape kwa Allaah na kwa damu ya ukaraba, hakika sisi tunakula “Al-‘Ilhiza”, yaani manyoya ya wanyama na damu (kinaya kuashiria hali mbaya sana ya njaa iliyowapata). Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

Ar-Rahm: (Ukaraba wa damu) uliyopo kati yao na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa atawaondoshea vikwazo vya chakula alivyowaekea Thumaamah bin Uthaal Al-Hanafiy ambaye alikuwa ni Wali wa Al-Yamaamah nchini Yemen. Aliposilimu, alizuia vyakula kupelekwa Makkah mpaka kwa idhini toka kwa Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 35

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾

35. Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake; Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu”. [Al-Ahzaab (33): 35]

 

Sababun-Nuzuwl: 

حَدَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ حُسَيْنٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ أُمِّ عُمَارَةَ الأَنْصَارِيَّةِ، أَنَّهَا أَتَتِ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ مَا أَرَى كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ لِلرِّجَالِ وَمَا أَرَى النِّسَاءَ يُذْكَرْنَ بِشَيْءٍ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ‏:‏ ‏ إن الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ‏ الآيَةَ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ وَإِنَّمَا يُعْرَفُ هَذَا الْحَدِيثُ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ

Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Muhammad bin Kathiyr, ametuhadithia Sulaymaan bin Kathiyr, toka kwa Huswayn, toka kwa ‘Ikrimah, toka kwa Ummu ‘Ammaarah Al-Answaariyyah kuwa alimwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na kumwambia: Sioni kila kitu isipokuwa ni kwa wanaume tu, na sioni wanawake wakitajwa kwa lolote. Hapo ikateremka Aayah hii: