Vitoweo
Kuku Wa Sosi Ya Ukwaju Wa Kuchomwa Katika Mkaa Na Saladi Ya Orzo

Vipimo
Kuku (miguu na paja) Safisha, osha kwa chumvi na siki atoke harufu - 12 mapande
Tangawizi mbichi iliokatwakatwa - 1 kipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) Menya- 1 uwa zima
Pilipilimbichi - 6
Pilipili mbuzi - 3
Ukwaju iliprowekwa na kukamuliwa - 1 kikombe cha chai
Bizari ya pilau/jiyra/cumin - 1 kijiko cha chai
Bizari ya gilgilan/Dania/coriander - 1 kijiko cha chai
Bizari ya manjano/haldi/tumeric - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 2
Namna Ya Kupika:
- Chanachana (slit) mapaja ya kuku kwa ajili ya kuingiza masala.
- Katika mashine la kusagia (blender) weka tangawizi mbichi, kitunguu thomu, pilipili mbichi na mbuzi, bizari zote, chumvi na ndimu.
- Saga hadi ilainike.
- Weka kuku katika bakuli umimine mchanganyiko wa masala. Changanya vizuri kuku aingie masala kila mahahli.
- Roweka (marinate) kwa muda wa masaa mawili au zaidi, huku unageuzageuza akolee pande zote.
- Choma katika mkaa hadi aive.
- Epua kulia na saladi ya orzo
Upishi wa saladi ya Orzo unapatikana katika kiungo kifuatacho:
Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki (Greek Orzo Salad)
Kidokezo:
Unaweza kuroweka tokea usiku ukaweka katika friji, ikiwa unataka kipimo kingi kwa kuongezea vipimo vya masala.