Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 38-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Anayetokwa Majimaji Je Inasihi Aswali Qiyaamul-Layl Kwa Wudhuu Wa ‘Ishaa?

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

38-Anayetokwa Majimaji Je Inasihi Aswali Qiyaamul-Layl Kwa Wudhuu Wa ‘Ishaa?

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Je inasihi kwa mwanamke huyu (anayetokwa majimaji) kuswali Qiyaamul-Layl itapokatika nusu ya pili ya usiku kwa wudhu wa ‘Ishaa?

JIBU:

Hapana, itakapokatika usiku wa nusu ya pili inapasa  kuchukua wudhu  mwingine.  Na imesemwa pia halazimiki kurejea kuchukua wudhu, na  hii ndiyo rai iliyokubaliwa.