Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 39-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ni Upi Muda Wa Mwisho Wa Swalaah Ya ‘Ishaa Na Vipi Kuujua

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

39-Ni Upi Muda Wa Mwisho Wa Swalaah Ya ‘Ishaa Na Vipi Kuujua

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Ni upi muda wa mwisho wa Swalaah ya ‘Ishaa, na vipi kuujua muda wenyewe?

JIBU:

Mwisho wa wakati wa ‘Ishaa ni katikati ya usiku na wakati wenyewe unaweza kuujua kwa kuugawa kati ya muda wa Magharibi na muda wa Swalaah ya Alfajiri. Nusu ya kwanza inaisha wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa. Na nusu ya pili inayobaki haikadiriwi kwa wakati bali kwa kitenganisho baina ya ‘Ishaa na Alfajiri.