Skip to main content

Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Fataawaa: Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas 59-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akiwa Katika Hedhi Baada Ya Jamarah Kabla Ya Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Hawezi Kurudi Baada Ya Safari

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

59-Akiwa Katika Hedhi Baada Ya Jamarah Kabla Ya

Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Hawezi Kurudi Baada Ya Safari

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Mwanamke akiwa na hedhi baada ya Jamarah (Kurushwa vijiwe) katika Al-‘Aqabah na kabla ya Twawaaf Al-Ifaadhwah, nae akiwa katika kundi pamoja na mumewe na marafiki wake, juu yake ni nini afanye pamoja na elimu ya kuwa hawezi kurejea baada ya safari yake?

JIBU:

Kama hawezi kurudi basi atajihifadhi vizuri kisha atatufu kwa hali ya dharura wala isiwe kitu juu yake, na kukamilisha baki ya ‘ibaadah za matendo ya Hijjah.