Maandazi Ya Kukandiwa Kwa Tui La Nazi Na Jinsi Ya Kuyahifadhi

Maandazi Ya Kukandiwa Kwa Tui La Nazi

    

 

Vipimo

 

Unga - 5 Vikombe

Tui la Nazi zito vugu vugu - 1 ¼ kikombe

Sukari  -  3/4 kikombe cha chai

Samli iliyoyayushwa au mafuta - 3 vijiko vya Supu

Hamirah - 2 Vijiko vya Supu

Hiliki -  1/2 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia

                                          
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya   kulia vya tui. Weka kando  mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
  2. Pasha samli moto
  3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki  na  samli ikiwa bado moto moto.
  4. Mimina hamira  ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza tui. Kanda unga mpaka uwe laini.
  5. Kata madonge *12 au 15  uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.

     *Ukipenda  maandazi  manene fanya madonge 12.  Ukipenda mepesi fanya madonge 15

   

 

  

6. Madonge yakifura, sukuma kama chapati kisha ukate mara nne kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo na madonge yote. Yawache maandazi yafure tena baada ya kukata kama dakika 15 takriban

 

 

7.    Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.

8.   Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.                                                                                                                                                                                        

 

   

 

Jinsi Ya Kuhifadhi Maandazi

 

  1. Unaweza kuweka unga wa maandazi uliokwishakanda au ambayo umeshayakatakata na yakaaumuka ndani ya freezer ikiwa unataka kutumia siku nyengine. Tumia waxed paper na unga wa kutosha kuweka katikati ya madonge au baina ya maandazi uliyokatakataka ili yasishikane unapoya freeze katika freezer.  Yakishika barafu, toa na yafunike kwa wax paper kiasi kama matano pamoja na uyatie katika freezer bags.  Ukitaka kukaanga maandazi siku nyengine, toa mdonge mapema kidogo  yatoke barafu kidogo tu kisha katakata uyakaange. Na ikiwa ni yale uliyokwishakatakata, yatoe yatokea barafu yaumuke tena kidogo kisha kaanga katika mafuta yamoto.  
  2. Vile vile unaweza kuyapika kabisa na kuweka katika freezer bags, ukitaka kutumia ni kuyatoa tu na kupasha moto katika Microwave, ila aina ya kwa kwanza ya kuhifadhi madonge ni bora zaidi.

   

 

 

Share