Skip to main content

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

Alhidaaya.com

 الصَّمَدُ

الصَّمَدُ

As-Swamad:

Mwenye Kukusudiwa Kwa Haja Zote

Allaah (سبحانه وتعالى), Yeye Ndiye Pekee Ambaye viumbe wote wanamtegemea kwa mahitaji yao yote; dhiki zao, mtihani, balaa na mashaka yao, na mahitaji yao yote mengineyo. Haya ni kutokana na ukamilifu Wake usio na mipaka wa Nafsi, Majina, Sifa na Matendo Yake.

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: Yeye ni Allaah Mmoja Pekee. 

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

Allaah ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote.  [Al-Ikhlaasw (112): 1-2)]