Skip to main content

Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa - أَحاديثُ عَنْ فَضْلِ الْعِلْم وَالْعُلَمَاء11-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Allaah Amneemeshe Mtu Anayebalighisha Risala Kama Alivyosikia

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

Hadiyth Ya 11

Allaah Amneemeshe Mtu Anayebalighisha Risala Kama Alivyosikia

Alhidaaya.com

عن إبْنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) ِ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَه، فَرُبَّ مُبَلِّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ)) وراوه الترمذي وقَالَ : حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ  

Imepokelewa toka kwa ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)   ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  akisema: ((Allaah Amneemeshe mtu aliyesikia kitu kutoka kwetu naye akakifikisha kama alivyosikia. Huenda anayefikishiwa akawa mwenye kufahamu zaidi kuliko aliyesikia)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]