12-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Aliyekuwa Umahiri Wa Qur-aan Yupamoja Na Malaika Anayejifunza Ana Thawabu Mara Mbili

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 12

Aliyekuwa Umahiri Wa Qur-aan Yupamoja Na Malaika,

Ama Anayejifunza Ana Thawabu Mara Mbili

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ))  

   

 'Aaishah  (رضي الله عنها) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)   amesema: “Yule aliyekuwa mahiri (mwenye ujuzi) wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa  atapata ujira mara mbili))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share