Skip to main content

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبة - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji025-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji:Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

Alhidaaya.com

Adabu Za Kula

025-Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

9- Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa

Toka kwa Jaabir:

"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِلَعْقِ الْأَصَابِعِ وَالصَّفْحَةِ ، وَقَالَ : "إِنَّكُمْ لَا تَدْرُونَ: فِي أَيَّهِ الْبَرَكَةُ؟ ".

Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kulamba vidole na sahani kwa kusema: “Hakika nyinyi hamjui wapi ilipo baraka yake”. [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2033)].