Skip to main content

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبة - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji024-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kulila Tonge Likianguka Baada Ya Kulipangusa Uchafu

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

Alhidaaya.com

Adabu Za Kula

024-Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu

8-  Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu

Toka kwa Jaabir amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأْخُذْهَا ، فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنَ الأَذَى وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْهَا لِلشَّيْطَانِ‏"

“Likianguka tonge la mmoja wenu basi aliokote, kisha alipanguse uchafu uliolipata na alile, na wala asiliache kwa shaytwaan.”  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2033)].