10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Akae Kuzungumza Na Mkewe Na Asikilize Mazungumzo Yake Kwa Hima
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
09: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 6-Akae Kuzungumza Na Mkewe Na Asikilize Mazungumzo Yake Kwa Hima:
Tunamwona Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakaa kumsikiliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) akimhadithia mazungumzo ya wanawake 11 waliokuwa wamekaa na kupeana ahadi ya kwamba hakuna yeyote kati yao atakayeficha habari yoyote ya mumewe na maisha wanayoishi. Mazungumzo haya yanajulikana kama kisa cha “Ummu Zar’i" ambacho ni kirefu. Lakini pamoja na urefu wake, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuchoka kumsikiliza ‘Aaishah akimhadithia visa vya wanawake hao 11 kuhusu waume zao mmoja baada ya mwingine hadi mwisho.
[Yaliyozungumzwa na wanawake hao kuhusu waume zao na hali wanayoishi nao, ndani yake kuna ahkaam za kisharia, adabu za unyumba, na mtangamano mwema wa mume kwa mkewe kwa mujibu wa Hadiyth hiyo ya ‘Aaishah ambayo tunasikitika kwamba hatukuifasiri kutokana na urefu wake].
