Al-Baariu: Mwanzilishi wa viumbe, Mwenye kutekeleza na kuleta katika uhai yale Aliyoyakadiria, bila ya kasoro, na kuvipambanua viumbe kila kimoja na umbo lake.
Jina hili tukufu limetajwa katika Qur-aan mara tatu (3). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾
Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi wa viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa. Kinamsabihi Pekee kila kilichoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Hashr (59:24)]
Na Kauli ya Nabiy Muwsaa (عليه السلام) kwa kaumu yake, ambayo imetaja Jina hili mara mbili:
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾
Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu, na ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumbaji wenu. Akapokea tawbah yenu, hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. [Al-Baqarah (2:54)]
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله) amebainisha tofauti ya Majina Al-Khaaliq na Al-Baariu:
الْخَلْقُ: التَّقْدِيرُ، وَالْبَرْءُ: هُوَ الْفَرْيُ، وَهُوَ التَّنْفِيذُ وَإِبْرَازُ مَا قَدَّرَهُ وَقَرَّرَهُ إِلَى الْوُجُودِ، وَلَيْسَ كُلُّ مَنْ قَدَّرَ شَيْئًا وَرَتَّبَهُ يَقْدِرُ عَلَى تَنْفِيذِهِ وَإِيجَادِهِ سِوَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ
“Al-Khalq ni kukadiria, na al-bar-u ni kutekeleza na kulileta katika uhai lile Alilolikadiria na kulipanga; na si kila anayekadiria kitu na kukipanga anaweza kukitekeleza na kukileta katika uhai, isipokuwa Allaah (عزّ وجلّ).”1
Na Imaam Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesema:
الْبَارِئُ وَالْمُصَوِّرُ تَفْصِيلٌ لِمَعْنَى اسْمِ الْخَالِقِ
“Al-Baariu na Al-Muswawwir ni ufafanuzi wa maana ya Jina Al-Khaaliq.”2
Maana Ya Al-Baariu:
1-Al-Baariu ni Mwanzilishi Anayeleta viumbe katika uhai; na neno hili limekuja katika Kauli Yake kuhusu Qadar Aliyoiandika kabla ya kuumba:
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾
Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla Hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi. [Al-Hadiyd (57:22)]
2-Al-Baariu Amevipambanua viumbe baadhi yake na baadhi; Amevitenganisha aina kwa aina, na Akakipa kila kiumbe umbo lake linaloendana na lengo la kuumbwa kwake.
3-Al-Baariu Ameumba viumbe Vyake bila ya kasoro wala mpasuko wowote. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾
Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka. Hutaona katika Uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho. Je, unaona mpasuko wowote ule? [Al-Mulk (67:3)]
4-Al-Baariu Amemuumba mwanaadam kutokana na ardhi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ ﴿٥٥﴾
Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine. [Twaahaa (20:55)]
5-Na neno lenye asili hii hii (ب ر أ) limekuja katika Qur-aan kwa maana ya kumtakasa mtu na tuhuma, kama Alivyomtakasa Allaah Nabiy Muwsaa (عليه السلام) na yale waliyomzulia:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾
Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliomuudhi Muwsaa, lakini Allaah Alimtoa tuhumani kutokana na yale waliyoyasema. Na alikuwa mbele ya Allaah mwenye kuheshimika. [Al-Ahzaab (33:69)]
6-Al-Baariu Ametakasika na kila upungufu na aibu katika Dhati Yake, Sifa Zake na matendo Yake, na Ametakasika na kufananishwa, kushirikishwa, kuwa na mke au watoto, na kila wanachomnasibishia makafiri.
Taathira Ya Imaan, Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah, Al-Baariu:
1-Tafakari Uumbaji Wa Al-Baariu:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Kutafakari uumbaji na Utukufu wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni miongoni mwa ‘ibaadah adhimu. Tafakari mbingu, jua, mwezi, nyota, ndege, wanyama, milima na bahari. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١١﴾
Huu ni Uumbaji wa Allaah, basi nionyesheni nini walichokiumba wasiokuwa Yeye. Bali madhalimu wamo katika upotofu bayana. [Luqmaan (31:11)]
Na Anasema pia:
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾ وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾ وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾ وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾
Je, hawawataamuli ngamia namna walivyoumbwa? Na mbingu vipi zilivyonyanyuliwa? Na milima vipi imekongomewa imara kabisa? Na ardhi vipi ilivyotandazwa? [Al-Ghaashiyah (88:17-20)]
2-Tambua Kwamba Al-Baariu Amekipa Kila Kiumbe Umbo Linalokifaa:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Kila kiumbe kimepewa umbo na uwezo unaokifaa kwa kazi yake, kisha kikaongozwa kwayo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾
(Muwsaa) akasema: Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza. [Twaahaa (20:50)]
3-Amini Qadar, Kwani Al-Baariu Aliandika Kila Kitu Kabla Ya Kuumba:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu, kwamba kila kitakachokufika kiliandikwa kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi; basi ridhika na usikate tamaa.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنهما) قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) يَقُولُ: ((كَتَبَ اللَّهُ مَقَادِيرَ الْخَلاَئِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ))
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Allaah Aliandika makadirio ya viumbe kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu hamsini.” [Muslim]
4-Mtii Al-Baariu Aliyekuumba, Wala Usimtii Yeyote Katika Kumuasi Yeye:
Kumbuka, ee Mja wa Al-Baariu, kwamba utiifu wako wa kwanza ni kwa Muumba wako; na hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Yeye.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
عَنْ عَلِيٍّ (رضي الله عنه) عَنِ النَّبِيِّ (صلى الله عليه وسلم) قَالَ: ((لاَ طَاعَةَ فِي مَعْصِيَةٍ، إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ))
Amesimulia ‘Aliy (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna utiifu katika maasi; hakika utiifu ni katika mema tu.” [Al-Bukhaariy] [Muslim]
5-Unapomuasi Allaah, Rudi Kutubia Kwa Al-Baariu:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Kama Nabiy Muwsaa (عليه السلام) alivyowaamrisha kaumu yake kutubia kwa Muumbaji wao; rejea Al-Baqarah (2:54) juu. Muumbaji wako Ndiye Anayekujua zaidi, na Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah.
6-Jitahidi Kuwa Miongoni Mwa Viumbe Bora:
Viumbe wote ni wa Al-Baariu, lakini walio bora kabisa kati yao ni wale walioamini na kutenda mema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio wema kabisa wa viumbe. [Al-Bayyinah (98:7)]
7-Mshukuru Al-Baariu Aliyekuumba Katika Umbo Bora Kabisa:
Tafakari umbo zuri Alilokuumbia Al-Baariu, na umshukuru kwa kulitumia katika kumtii.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾
Kwa yakini Tumemuumba binaadam katika umbile bora kabisa. [At-Tiyn (95:4)]
8-Nyenyekea, Kwani Asili Yako Ni Udongo:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Mwanaadam ameumbwa kutokana na ardhi, na atarudishwa humo, na atatolewa humo mara nyingine (rejea Twaahaa (20:55) juu); basi kuna nini cha kujivunia?
9-Usiwaudhi Waja Wema, Kwani Allaah Huwatetea Na Kuwatakasa Na Tuhuma:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Kama Alivyomtakasa Nabiy Muwsaa (عليه السلام) na yale waliyomzulia (rejea Al-Ahzaab (33:69) juu), Allaah Huwatetea Waumini. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ ﴿٣٨﴾
Hakika Allaah Anawalinda wale walioamini. Hakika Allaah Hampendi kila mwenye tabia ya kukhini, mwingi wa kukufuru. [Al-Hajj (22:38)]
10-Mwombe Al-Baariu Kwa Kukiri Kwamba Yeye Ndiye Aliyekuumba:
Tambua, ee Mja wa Al-Baariu: Du’aa hii inaitwa Sayyid Al-Istighfaar, na ndiyo du’aa bora kabisa ya kuomba maghfirah:
عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) عَنِ النَّبِيِّ (صلى الله عليه وسلم) قَالَ: ((سَيِّدُ الاِسْتِغْفَارِ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي، فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ. قَالَ: وَمَنْ قَالَهَا مِنَ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنَ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ))
Amesimulia Shaddaad bin Aws (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sayyid Al-Istighfaar (bwana wa istighfaar) ni useme:
اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي، فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ
Yaa Allaah! Wewe Ndiye Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe. Umeniumba nami ni Mja Wako, nami niko juu ya Ahadi Yako na agano Lako kwa kadiri ya uwezo wangu. Najikinga Kwako kutokana na shari ya niliyoyafanya. Nakiri Kwako Neema Yako juu yangu, na nakiri Kwako dhambi yangu; basi Nighufurie, kwani hakuna anayeghufuria madhambi isipokuwa Wewe. Akasema: Atakayeisema mchana akiwa na yakini nayo, akafa siku hiyo kabla ya jioni, basi yeye ni miongoni mwa watu wa Jannah. Na atakayeisema usiku akiwa na yakini nayo, akafa kabla ya asubuhi, basi yeye ni miongoni mwa watu wa Jannah.” [Al-Bukhaariy]
Na Allaah Mjuzi zaidi