Skip to main content
Majina Mazuri Ya Allaah Jina 080 kati ya 103
Al-Qahhaar — Majina Mazuri ya Allaah

Al-Qahhaar: Mwenye kudhibiti kila kitu kwa ukamilifu; Ambaye viumbe vyote vimemnyenyekea, na majabari wote wamedhalilika mbele Yake.

Jina hili tukufu limetajwa katika Qur-aan mara sita, na kila mara limeambatana na Jina Al-Waahid. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾

Sema: Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi? Sema: Ni Allaah. Sema: Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa rafiki walinzi na hali hawamiliki manufaa wala dhara kwa nafsi zao? Sema: Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru? Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha ukafanana uumbaji kwao (wakakanganyikiwa)? Sema: Allaah Ni Muumbaji wa kila kitu, Naye Ni Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ar-Ra’d (13:16)]

Na Anasema pia:

قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾

Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu. Na hakuna Muabudiwa wa haki yeyote isipokuwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Swaad (38:65)]

Maana Ya Al-Qahhaar:

1-Al-Qahhaar ni neno la kukithirisha kutoka katika Al-Qaahir; linaonyesha ukamilifu na wingi wa udhibiti wa Allaah juu ya kila kitu.

2-Kuambatana kwa Jina hili na Al-Waahid kunaonyesha kwamba Mmoja Pekee Ndiye Anayedhibiti kila kitu; na mwenye kudhibiti kila kitu hawezi kuwa na mshirika.

3-Udhibiti Wake utadhihirika kikamilifu Siku ya Qiyaamah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿٤٨﴾

Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine na mbingu pia, na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ibraahiym (14:48)]

Na Anasema pia:

يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿١٦﴾

Siku watakayotokeza wao, hakitofichika kitu chochote chao kwa Allaah. Ufalme ni wa nani leo? (Allaah Mwenyewe Atajijibu): Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Asiyepingika. [Ghaafir (40:16)]

Taathira Ya Imaan, Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah, Al-Qahhaar:

1-Mpwekeshe Al-Waahid Al-Qahhaar Katika ‘Ibaadah:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Qahhaar, kwamba Aliyeumba kila kitu na Kukidhibiti Ndiye Pekee Anayestahiki kuabudiwa (rejea Ar-Ra’d (13:16) juu).

2-Tumia Hoja Ya Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) Katika Kulingania Tawhiyd:

Tambua, ee Mja wa Al-Qahhaar, kwamba Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) aliwalingania wafungwa wenzake kwa Jina hili. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴿٣٩﴾

Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika? [Yuwsuf (12:39)]

3-Tafakari Siku Ambayo Viumbe Watajitokeza Mbele Ya Al-Waahid Al-Qahhaar:

Tafakari, ee Mja wa Al-Qahhaar, Siku ambayo ardhi na mbingu zitabadilishwa, na viumbe wote wakajitokeza mbele Yake (rejea Ibraahiym (14:48) juu).

4-Kumbuka Siku Ambayo Hakutakuwa Na Ufalme Isipokuwa Wa Al-Qahhaar:

Kumbuka Siku itakayoulizwa: Ufalme ni wa nani leo? Na jibu litakuwa: Ni wa Al-Qahhaar, Mmoja, Al-Qahhaar (rejea Ghaafir (40:16) juu).

5-Ukitaka Kuonya, Onya Kwa Al-Waahid Al-Qahhaar:

Tambua kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrishwa kujitambulisha kuwa ni muonyaji, na kwamba hakuna mwabudiwa isipokuwa Al-Waahid Al-Qahhaar (rejea Swaad (38:65) juu).

6-Tahadhari Na Kiburi, Kwani Al-Qahhaar Amewadhalilisha Majabari Wote:

Tahadhari na kujikweza; kila jabari aliyepita ameshindwa na kudhalilika mbele ya Al-Qahhaar. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّوْ أَرَادَ اللَّـهُ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا لَّاصْطَفَىٰ مِمَّا يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٤﴾

Lau Angelitaka Allaah kujichukulia mwana, Angelikhitari Amtakaye miongoni mwa Aliowaumba. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake), Yeye Ndiye Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Az-Zumar (39:4)]

7-Dhibiti Nafsi Yako Kabla Haijakudhibiti:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Qahhaar, kwamba ushindi mkubwa wa mja ni kuishinda nafsi yake na matamanio yake kwa ajili ya kumtii Allaah (rejea An-Naazi’aat (79:40-41) katika 079-Al-Qaahir).

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾ فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾

Ama yule aliyekhofu kisimamo mbele ya Rabb wake, na akaikataza nafsi yake na hawaa. Basi hakika Jannah ndio makaazi yake. [An-Naazi’aat (79:40-41)]

8-Kumbuka Mauti, Udhibiti Wa Al-Qahhaar Usiomwacha Yeyote:

Tambua, ee Mja wa Al-Qahhaar, kwamba mauti yamewadhibiti wafalme na mafakiri, wenye nguvu na wanyonge; na hakuna nafsi isiyoyaonja. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾

Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka. Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu. [Ar-Rahmaan (55:26-27)]

9-Mwamini Al-Qahhaar Kuwa Atanusuru Dini Yake:

Kumbuka, ee Mja wa Al-Qahhaar, kwamba hakuna nguvu inayoweza kushinda udhibiti wa Allaah; basi uwe na yakini kwamba Dini Yake itashinda. Rejea At-Tawbah (9:33) katika 011-Adhw-Dhwaahir.

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah (9:33)]

10-Mwombe Al-Qahhaar Nusura Dhidi Ya Maadui Wa Dini:

Omba du’aa, ee Mja wa Al-Qahhaar, kama alivyoomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) dhidi ya makundi yaliyoungana dhidi ya Waislamu:

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى (رضي الله عنه) قَالَ: دَعَا رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) عَلَى الأَحْزَابِ فَقَالَ: ((اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الْكِتَابِ، سَرِيعَ الْحِسَابِ، اهْزِمِ الأَحْزَابَ، اللَّهُمَّ اهْزِمْهُمْ وَزَلْزِلْهُمْ))

Amesimulia ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyaombea maangamizi makundi yaliyoungana (Al-Ahzaab), akasema:

اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الْكِتَابِ، سَرِيعَ الْحِسَابِ، اهْزِمِ الأَحْزَابَ، اللَّهُمَّ اهْزِمْهُمْ وَزَلْزِلْهُمْ

Yaa Allaah! Mteremshaji wa Kitabu, Mwepesi wa kuhesabu, yashinde makundi haya. Yaa Allaah! Washinde na Uwatikise. [Al-Bukhaariy] [Muslim]

Na Allaah Mjuzi zaidi