Katlesi Za Kuku Mviringo Wa Yai

Katlesi Za Kuku Mviringo Wa Yai

Vipimo na namna ya kutayarisha

Mbatata/viazi Chemsha - 2 Kilo

Kuku safisha, osha  katakata vipande - ½ 

Mayai Piga kwa uma (fork katika kibakuli) - 3

Vitunguu maji katakata vidogodogo (chopped) - 2

Pilipili shamba/mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Ndimu/limau Kamua - 1 au mbili

Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

Tangawizi mbichi Saga - 1 kipande

Kitunguu thomu (saumu) Saga - 7 – 10 chembe

Uzile/bizari nyembamba/ya pilau/cumin Saga - 2 vijiko vya chai

Bizari ya mchuzi ukipenda = 1 kijiko cha chai

Kotmiri majani osha, katakata (chop) = 1 kikombe

Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani ya chali - 1 kikombe

Namna Ya Kupika:

  1. Menya mbatata/viazi
  2. Chemsha kuku kwa tangawizi na kitunguu thomu, ndimu, au limau mpaka akauke
  3. mchambue kuku mtoe mifupa
  4. Ziponde mbatata katika bakuli mpaka zivurugike.
  5. Changanya vizrui na mbatata/viazi, kuku na viungo vyote vinginevyo isipokuwa chenga za mkate na mafuta, na mayai
  6. Fanya madonge uviringe kama shepu ya yai.
  7. Chomva katlesi ndani ya mayai halafu karagiza kwenye bread crumbs.
  8. Weka mafuta yashike moto, zitie katelsi mpaka zigeuke rangi ya dhahabu zitowe tayari kwa  kuliwa. 

 

 

 

 

Share