Aliyesilimu Akaritadi Anaweza Kurudi Katika Dini Ya Kiislamu?

SWALI:

 

Mtu  aliyesilim  kutoka kwenye dini ya kweli kisha baada ya muda fulani akataka kurudi anaruhusiwa?   

  

JIBU:

 Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Mtu ambaye alikuwa ni Muislamu kisha akaritadi anaweza kurudi katika Dini anapoona kuwa amefanya makosa. Na jambo hili lilitokea wakati wa Sayyidna Abu Bakar (Radhiya Allaahu ánhu) ambapo Waarabu waliritadi na baadae wakarudi katika Dini yao ya asili. Na ni makosa makubwa sana kwa mtu kufanya kitendo hicho cha kuingia na kutoka katika Dini kwa dhihaka au istihzai. Lakini likifanywa mara nyingi litamletea matatizo makubwa sana mtu mwenyewe kwani litamuingiza katika ukafiri. Allah Anasema:

Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Allaah  hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia(4: 137).

Share